Kapombe akiwa Ufaransa kabla ya kurejea nchini |
Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
Imechapishwa Juni 10, 2014, saa 3:13 usiku
SHOMARY Kapombe amesema ubora wa wachezaji na
makocha wa mabingwa wa ligi kuu soka Tanzania bara, Azam fc ndio sababu kubwa yeye kuchagua
kujiunga na klabu hiyo kuelekea msimu mpya wa ligi kuu unaotarajia kuanza
kushika kasi mwezi Agosti mwaka huu.
Siku za karibuni, beki huyo kiraka aliamua kusaini
mkataba wa miaka mitatu Azam fc na ataitumikia klabu hiyo msimu ujao wa ligi
kuu na michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika.
Kapombe alisema kucheza Azam fc kwasasa ni salama
kuliko klabu yoyote ya Tanzania kwani wanalipa vizuri na wanawajali wachezaji
kwa kila kitu.
Aliongeza kuwa Azam imejikamilisha kwa kila kitu
kuanzia uwanja na vifaa vya mazoezi.
Aidha Kapombe alisema yeye anapenda ushindani
katika soka, hivyo anapenda kucheza timu
yenye wachezaji wakali.
“Azam kuna ushindani mkubwa. Binafsi sipendi
kucheza timu isiyo na ushindani. Kama kuna ushindani, kunanifanya nifanye
mazoezi sana”. Alisema Kapombe.
Pia alikiri kujawa na furaha baada ya kurudi
nyumbani na hususani klabu bora ya Azam fc na anaamini timu hiyo itarudisha
makali yake.
0 comments:
Post a Comment