Na Boniface Wambura, Dar es salaam
Maziko ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira
wa Miguu Tanzania (TFF) wakati huo likiitwa FAT, Kanali mstaafu Ali Hassan
Mwanakatwe yanafanyika leo (Juni 10 mwaka huu) Magugu, Babati mkoani Manyara.
Kanali Mwanakatwe alifariki dunia Juni 7 mwaka huu
katika Hospitali Kuu ya Jeshi (GMH) Lugalo jijini Dar es Salaam wakati
akipatiwa matibabu baada ya kuanguka bafuni nyumbani kwake Mbezi Beach.
TFF imetoa ubani wa sh. laki tano kwa familia ya
marehemu Kanali Mwanakatwe, na katika maziko hayo inawakilishwa na mjumbe wa
Kamati ya Utendaji wa Kanda ya Arusha na Manyara, Omari Walii.
0 comments:
Post a Comment