Imechapishwa Juni 6, 2014, saa 12:10 jioni
Bondia Julias kisarawe kesho anategemea kupanda
ulingoni kuzipiga na Hassan kiwale “Morobest” katika ukumbi wa Friends
Corner Manzese jijini Dar es salaa. Pambano hilo kali litakuwa la raundi
nane.
Akizungumza na vyombo vya habari , muandaaji wa
pambano hilo, Sempai Gola na ofisa wa ngumi za kulipwa nchini, Pembe
Ndava kwa pamoja walisema maandalizi yote yamekamilika na mabondia wapo katika
hali nzuri ukiondoa kasoro ndogo iliyojitokeza kwa Moro Best ambaye alitakiwa
acheze na Fadhili Majia na sasa atacheza na Julias Thomas kisarawe ambaye ni
mbadala mkali kwani bondia huyo hajapoteza mchezo katika michezo yake kumi na
mbili aliyocheza.
Pambano hilo linategemewa kuanza jioni mida ya
saa kumi na kutakuwepo na mapambano mengi mno ya utangulizi.
0 comments:
Post a Comment