Saturday, June 7, 2014

hans-poppe
Na Baraka Mbolembole
Fundi ni mwenye mali au mjenzi?. Siku kadhaa zilizopita, mshambuliaji wa klabu bingwa ya Tanzania Bara, Azam FC, Muivory Coast, Kipre Tcheche alitwaa tuzo ya mwanasoka bora wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara. Kipre ambaye alijiunga na Azam, januari, 2011 ametwaa tuzo hiyo ya msimu wa 2013/14 baada ya kuonesha kiwango kikubwa uwanjani. Ukitoa magoli 13 aliyofunga, mfungaji huyo bora wa mwaka 2013, alijitofautisha na wachezaji wengi wa kigeni ambao wamekuwa wakitua katika soka la Tanzania. Huyu ni mchezaji wa kulipwa hasa, na hata klabu yake itakuwa inafahamu mchango wake ndiyo maana ameshikilia chati ya wachezaji wanaolipwa mshahara mkubwa katika soka la Tanzania.
Kwa nini Kipre na isiwe, Emmanuel Okwi, mchezaji aliyeingiza kiasi kikubwa cha pesa katika muda wa miezi miwili tu? Kamati za usajili za klabu zina watu sahihi?, je ni watu wenye ufahamu kuhusu aina ya wachezaji ambao klabu zao zinaweza kuwafaa?. Juzi, mwenyekiti wa kamati ya usajili wa klabu ya Simba Zacharia Hans Poppe amechimba mkwara kuwa mtu yoyote asipokee pesa za malipo ya usajili wa mchezaji, Shomari Kapombe kutoka kwa Azam FC ambao wamefanikiwa kumsaini mchezaji huyo wa zamani wa Simba ambaye aliondoka nchini mapema mwaka uliopita kwenda nchini Ufaransa kujiunga na klabu ya daraja la nne ya AS Cannes kwa kile kilichotajwa ni usajili wa mkopo wa muda mrefu- miaka miwili.
Acha na mambo ya pesa, unajiuliza tu, je , Simba walikuwa na sababu yoyote ya kufikia maamuzi yale kwa mchezaji ambaye alikuwa na umri chini ya miaka 21?. Kama lengo ilikuwa ni kumuendeleza mchezaji huyo kisoka, Simba ingeweza kufanya kama ilivyokuwa kwa Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini ambao walimuuza mchezaji Knowledge Musona kwa klabu ya Homfeim ya Ujerumani lakini mchezaji huyo aliposhindwa kutulia nchini Ujerumani alirudi bure klabuni hapo baada ya miaka miwili. Musona ndiyo kwanza ana umri wa miaka 23, hivyo timu hiyo ya Afrika Kusini inaweza kumuuza tena baadaye kwa kitita kikubwa.
Lakini katika hili la Kapombe na mazingira yake namna yalivyo kwa sasa ni kama iliandaliwa mipango ambayo mwisho wake ni viongozi wa Kamati ya usajili kutangaza kuwa kiongozi yoyote asipokee pesa ya wanunuzi Azam. Kwa makubaliano yalivyo kati ya klabu za Simba na Cannes ni kuwa, Wafaransa hao wanatakiwa kuilipa Simba asilimia 40 ya malipo ambayo watamuuza mlinzi huyo kwa klabu yoyote. Na Azam wamefanikiwa katika hilo baada ya kuipatia Cannes kiasi cha euro zaidi ya 100, 000, hivyo asilimia 40 ya Simba ni kiasi kinachofikia dolla 40, 000. Je, hii ni biashara nzuri kwa nani?
Ni kweli, Simba imenufaika na malipo ya mchezaji huyo?. Hii ni moja kati ya kazi za kamati za usajili za klabu. Kwanza huuza wachezaji kwa mitazamo yao binafsi huku wakitegemea sehemu ya malipo hayo kufanya mambo yao binafsi kitu ambacho hakipaswi kuendelea kuwepo katika nyakati hizi . Poppe alishasema kuwa hatosaini mchezaji yoyote hadi Evance Aveva na Geofrey Nyange Kaburu washinde katika uchaguzi mkuu ujao. Alikuwa akimaanisha kuwa hayupo tayari kufanya kazi na mtu mwingine kwa sababu haendani nao. Kivipi?, Poppe yeye ana mtazamo gani kwa klabu ambao wagombea wengine hawana?
KAPOMBEUFARASAAmechimba mkwara kwa kuonya kuwa yeye ndiye anahusika na kila kitu kuhusu uuzwaji wa Kapombe, Ufaransa na hivyo anafahamu kila kitu. Sikatai lakini yeye ni kama nani hasa katika klabu? Je, saini inayotakiwa kuwepo katika karatasi za malipo huwa ni za mwenyekiti wa kamati ya usajili au mwenyekiti na mtendaji mkuu wa klabu?. Maneno yake yote ambayo amekuwa akiyazungumza katika siku za karibuni yamezidi kumvunjia heshima yake, watu wa mpira wanaanza kupoteza imani naye na itafikia wakati ataweka wazi kila kitu kuhusu namna alivyo na nguvu ndani ya Simba. Anawataka marafiki zake kwa madai kuwa wanaendana, kivipi, anajua mwenyewe ila inatakiwa ifikie wakati waiache klabu isimame yenyewe.
Simba ni taasisi kubwa, Simba inatakiwa na makampuni kibao ambao yanataka kujitangaza katika taasisi hiyo inayofuatiliwa na kupendwa na watu wengi nchini. Lakini yote haya hayawezi kuwepo kwa kuwa klabu inaendeshwa katika taratibu zisizokuwa na taswira ya kimaendeleo ndani na nje ya uwanja. Suala la Kapombe linaweza lisionekane athari zake lakini ndani ya uwanja limeiathiri timu. Kapombe alikuwa mchezaji muhimu katika safu ya nyuma pia alikuwa na maendeleo mazuri ya kiuchezaji , lakini timu ambayo haikujua chochote kuhusu alipotoka mchezaji huyo, miaka miwili iliyopita imeingia mamillioni ya shilling baada ya kukaa na mchezaji huyo kwa miezi isiyozidi sita!
Wakati pesa ikiwa karibu kutoka –kiongozi wa kamati ya usajili ndiye anataka kuchukua pesa hizo yeye, kwa madai kuwa zitasaidia kusajili wachezaji wengine kwa ajili ya msimu ujao. Najiuliza tu hapa na sipati majibu. Mtu huyu tayari amesema hatofanya kazi na kiongozi mwingine yoyote endapo Aveva na Kaburu wataanguka katika uchaguzi, sasa hizo pesa akipewa na jamaa zake wakaanguka itakuwaje?
Juzi, Mbeya City imeingia mkataba wa million 360 na kampuni ya Binslum, hiyo ni dalili ya klabu hiyo kuwavutia watu na hapo ndipo makampuni mbalimbali hujitokeza kwa nia ya kujitangaza. Kizuri kinajiuza, na kibaya kinajitembeza, Poppe anajaribu kujitangaza kwa mazuri yake huku akijinadi kuwa amekuwa akitumia pesa zake nyingi kuisaidia klabu hiyo. Anasahau kuwa upande wa pili kuna matatizo mengi ambayo wameisababishia klabu.
Ndani ya uwanja maamuzi kama ya kuwasaini wachezaji, Lino Musombo, Kanu Biyavanga, Kommabil Keita, Paschal Ocheng, Danniel Akkufor ulikuwa ni mbaya. Kwa kuwa wachezaji hao walisajiliwa bila kuwa na mtazamo wa kiufundi na utamaduni wa klabu. Labda, Keita, lakini kati ya wachezaji hao wa kigeni waliopewa pesa nyingi hakuna mwingine ambaye anaendana na tamaduni ya kiuchezaji wa klabu hiyo.
Wachezaji bora wameuzwa pasipo kuangalia faida ya kibiashara na kiuchezaji kwa klabu matokeo yake wachezaji kama Mwinyi Kazimoto, Kapombe na Emmanuel Okwi wameondoka wakiwa vijana na klabu imepata kiasi kiduchu tu . Okwi ni mchezaji hasa wa Simba, kama ilivyo kwa Kapombe na Kazimoto, ila kwa wote watatu klabu haijapata zaidi ya million 100. ‘ Jicho langu la Tatu’ halioni umuhimu wa kamati za usajili za klabu badala yake ni lazima wawepo mascout wa klabu ambao wanaweza kuwa wachezaji wa zamani wa timu husika .
Wachezaji bora kama Kipre walionesha viwango vyao wenyewe, ila ile migharasa imekuwa sehemu ya upatikanaji pesa kwa baadhi ya wahusika katika kama za usajili za klabu kubwa. Simba inatakiwa kusajili kwa pesa zake yenyewe, Simba inatakiwa kusukwa na wachezaji wa zamani wa klabu ambao watahusika kusaka vipaji ambavyo vitaendana na utamaduni wa kiuchezaji wa klabu hiyo. Fundi ni mwenye mali na si mjenzi, Pole, Poppe unataka hadi pesa kiduchu za Kapombe?. Saini yako itasimama kama nani?. Nauliza, je kuna sababu ya kuwepo kwa kamati za usajili katika klabu ?. Mimi jibu langu hapana, Simba inaweza kuwatua wadhamini na akaunti yake ikawa inatuna, wasaka vipaji wakiwasaidia kutafuta wachezaji wa Simba- hasa. Baada ya Okwi, Simba imepigwa bao lingine katika usajili wa Kapombe. Mchezaji kinda kijana mwenye ubora aliyeingiza pesa kiduchu. 0714 08 43 08

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video