Tabasamu tu: Michael Richard Wambura amemfunga bao tamu mwanasheria Dkt. Damas Ndumbaro baada ya kamati ya Rufani ya TFF kumrudisha, sasa vita ni kati yake na Evanc Aveva kwenye king`anyiro cha Urais katika uchaguzi wa juni 29 mwaka huu.
Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
Imechapishwa Juni 11, 2014, saa 11:05 jioni
SAA chache baada ya kamati ya Rufani ya shirikisho
la kandanda Tanzania, TFF, chini ya mwenyekiti wake, Wakili Julius Mutabazi
Lugaziya kumrudisha, Michael Richard Wambura kwenye uchaguzi wa Simba sc,
mgombea huyo amesema sasa haki imetendeka na uchaguzi utakuwa wa amani.
Wambura amezungumza na mtandao huu dakika chache
zilizopita na kusema kuwa anaufananisha ushindi wake kama mchezo wa mpira wa
miguu.
“Mpira wa miguu una mechi ya nyumbani na
ugenini, unaweza ukafungwa ugenini,
ukashinda nyumbani, bila kujali umeshinda goli ngapi, lakini ninachoweza kusema
ni kwamba haki imetendeke, matokeo yametoka, tujipange kwenda kwenye uchaguzi ili
wanasimba wapate viongozi wao wanaowataka”. Amesema Wambura.
Mgombea huyo ameongeza kuwa hiki sio kipindi tena
cha kutafuta mchawi, bali ni kipindi kinachohitaji wanasimba kuwa makini.
“Ni kipindi cha kuwa makini, kuweka sera zetu
hadharani, malengo yetu hadharani, ili wana Simba wapate fursa ya kuchagua kwa
sera, nadhani hilo ndio ombi langu”. Ameongeza Wambura.
Hata hivyo, Wambura amesema kesho ataongea na
waandishi wa habari makao makuu ya klabu ya Simba mtaa wa Msimbazi, kariakoo
jijini Dar es salaam.
0 comments:
Post a Comment