Hotuba ya Mkurugenzi wa Binslum Tyre Company Ltd, Ndugu
Mohamed Binslum siku ya utiaji sahihi mkataba wa udhamini wa Timu ya
Mpira wa Miguu ya Mbeya City jijini Mbeya.
Ndugu mgeni rasmi, Mheshimiwa Meya Wa Jiji La Mbeya
Mheshimiwa Mkurugenzi wa jiji
Mwenyekiti wa Timu ya Mbeya City
Wageni waalikwa
Mabibi na mabwana
Kampuni ya Binslum Tyre Company Limited inatambua umuhimu wa mpira wa
miguu hapa nchini ambao ni maarufu sana duninani kote, Udhamini huu
ambao ni wa kwanza kwa Kampuni yetu kudhamini timu za nje ya Dar Es
Salaam unalenga kuiimarisha timu ya Mbeya City ili kufanya vizuri zaidi
katika ligi kuu kwa misimu ijayo. Pia kuendeleza mpira wa miguu hapa
jijini na Tanzania Kwa ujumla.
Kwa kutambua hilo tumeamua kuidhamini timu ya mpira wa miguu ya Mbeya
City ya jijini hapa kwa mkataba wa miaka miwili wenye thamani ya
shilingi za kitanzania milioni mia tatu na sitini (360,000,000).
Betri zetu za RB zitakuwa wadhamini, kwa maana hiyo tutatangaza betri
zetu za RB katika jezi za timu ya Mbeya City, Betri za RB Zipo za aina
tofauti tofauti kulingana na uwezo wa gari na zinapatikana hapa jijini
Mbeya katika maduka mengi. Binslum Company Tyre Company Limited ina
bidhaa nyingi kama matairi, betri, rim za matairi na mipira.
Napenda
kuwashukuru viongozi wa Mbeya City, Meya wa jiji, Mkurugenzi na
Viongozi wote wa Timu kwa kuonyesha ukomavu katika uongozi wa mpira wa
miguu, na hilo pia ndio jambo muhimu na limetuvutia kufanya makubaliano
haya ya msingi ya kuidhamini timu ya Mbeya City. Pia ni njia mojawapo ya
kuitikia wito wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Jakaya
Mrisho Kikwete kuhusu makampuni kujikita katika kudhamini michezo
mbalimbali hapa nchini.
Mwisho naomba kutoa shukrani za dhati kwa Meya wa jiji la Mbeya kwa
kuunda timu nzuri na pia wananchi wa Mbeya kuithamini na kuishangilia
timu yao kila inapokwenda, nina imani mtakuwa mabalozi wazuri katika
kuitangaza betri ya RB.
Ahsanteni sana.
0 comments:
Post a Comment