Kwaheri: David Villa amewaaga Atletico Madri.
Imechapishwa Juni 2, 2014, saa 1:47 usiku
KLABU ya New York City FC imekamilisha
usajili wa mshambuliaji wa kimataifa wa Hispania, David Villa kwa
mkataba wa miaka mitatu.
Klabu
hiyo kubwa inayomilikiwa na
Manchester City na New York Yankees, imethibitisha katika mtandao wake
wa Twita kuwa nyota huyo mwenye miaka 32 ni mchezaji wao mkubwa wa
kwanza kumsajili.
Klabu ilitweet: "Karibu
New York City: David Villa (@Guaje7Villa) rasmi amesaini kama mchezaji
wa kwanza mkubwa kusajiliwa na £NYCFC. £VillatoNYCFC.'
Villa anakwenda Marekani baada ya kuwasaidia Atletico Madrid kushinda taji lake la kwanza tangu mwaka 1996 na kufika fainali ya UEFA ambapo walipoteza dhidi ya Real Madrid.
Nyota huyo alijiunga na Atletico majira ya kiangazi mwaka 2013 baada ya kucheza misimu mitatu ya mafanikio katika klabu ya Barcelona, wakati huo huo aliwahi kuzichezea Valencia, Real Zaragoza and Sporting Gijon.
0 comments:
Post a Comment