Sunday, June 15, 2014



http://4.bp.blogspot.com/-9Wfzmq5HqVo/UnPFaQmOqMI/AAAAAAAA6XU/Qw_4RUP1sJk/s1600/02.jpg
Nimewaua!: Mshambuliaji wa Yanga sc, Jerryson Tegete ( wa kwanza kushoto) akishangilia moja ya bao lake msimu uliopita na wachezaji wenzake, Mrisho Ngassa (katikati) na Saimon Msuva (kulia).

Na Baraka Mpenja, Dar es salaam

Imechapishwa Juni 15, 2014, saa 8:40 mchana

MSHAMBULIAJI wa Yanga sc, Jerryson John Tegete amefurahishwa na viwango vya timu zinazoshiriki kombe la dunia mwaka huu nchini Brazil japokuwa bado michuano ni mibichi kabisa.
Tegete amezungumza na MPENJA BLOG mchana huu na kueleza kuwa Cameroon ilianza kwa kufungwa na Mexico bao 1-0, lakini walikuwa na nafasi ya kufanya vizuri.
“Timu za Afrika zimejiandaa vizuri. Cameroon wangekuwa makini wangefaya vizuri”. Alisema Tegete.
“Nimewaona Ivory costa wakicheza, sio wabaya, kuna makosa machache wanafanya na wanapoteza nafasi nyingi, lakini nadhani wawakilishi wa Afrika watafanya vizuri tu”.
Tegete aliongeza kuwa kitu alichojifunza kwa mechi hizi za mwanzo ni timu kucheza kitimu zaidi na si mchezaji mmoja mmoja, jambo ambalo amelipenda na angetamani wachezaji wenzake wajifunze.
Pia amekiri kuw ajuzi hauzeeki baada ya kiungo mkongwe wa Italia, Andrea Pirlo kuonesha kandanda safi kwenye mchezo dhidi ya England.
“Nimefurahishwa sana na kiwango cha Pirlo katika, unaona alivyocheza vizuri jana, hili ni fundisho kuwa ukiwa na nidhamu ya mpira, utaucheza kwa muda mrefu”.
 In control: Pirlo keeps the ball from Daniel Sturridge
Pirlo amezidi kuonesha utaalam wake licha ya umri kumuacha

“Pia bao la Van Persie nimelipenda sana. Alifunga wakati muafaka, alijituma na kuisaidia Uholanzi. Aliuvaa unahodha wake. Ni fundisho zuri kwangu”. Alisema Tegete.
Pia nyota huyo wa Yanga alisema wachezaji vijana kama Neymar wameleta changamoto kubwa katika mashindano na kuyafanya yawe na mvuto.
Tegete ni moja ya washambuliaji walioibuliwa na Maximo akiwa kocha wa Taifa stars, na kama kweli kocha huyo atarejea nchini, basi Tegete anaweza kuzaliwa upya.
Kwa misimu miwili sasa, Tegete hajafanya vizuri akiwa na klabu yake ya Yanga, lakini alikiri kuwa majeruhi ya goti yamemsumbua kwa muda mrefu.
Mechi za mwishoni mwa msimu uliopita, Tegete alirudi katika kiwango kizuri sambamba na mshambuliaji aliyesajiliwa na Yanga kutokea klabu ya Mtibwa Sugar, Hussein Javu.
Tegete alisema kwakuwa amepona goti, msimu ujao atafanya vizuri na mpaka kurejea timu ya taifa ya Tanzania, Taifa stars chini ya kocha Mholanzi, Mart Nooij.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video