
Chumba cha kulala: Nyota wa Ureno, Joao Moutinho ameposti picha hii kwenye mtandao wa Twita akionesha chumba chake cha kulala nchini Brazil.
Imechapishwa Juni 12, 2014, saa 12:10 jioni
WAKATI
kitu cha kwanza atakachokiona Lionel Messi kila aamuka asubuhi ni
mchezaji mwenzake Sergio Aguero baada ya wawili hao kupangiwa chumba
kimoja cha kulala, Cristiano Ronaldo kwake ni tofauti kwani ataishia
kuiona picha yake kufuatia kupewa chumba cha peke yake.
Pengine
hili litakuwa jambo jema kwa Ronaldo aliyeshangilia bao la nne la Real
Madrid kwenye fainali ya UEFA baina ya Real Madrid dhidi ya Atletico
Madrid kwa kuvua jezi yake na kutunisha kifua chake.

Moutinho (kushoto) ana matumaini ya kuanza katika kikosi cha kwanza cha Ureno kwenye mchezo wa ufunguzi dhidi ya Ujerumani.

Mwanasoka bora wa dunia, Cristiano Ronaldo (kulia) alicheza kwa dakika 66 katika mechi ya kirafiki waliyoshinda mabao 5-1 dhidi ya Jamhuri ya Ireland
Ureno waliwasili katika kambi yao na kukuta wameshaandaliwa vyumba vya kulala vikiwa na majina ya wachezaji na kikosi kwenye vitanda vyao, pia kumewekwa picha zao ukutani.
Kiungo Joao Moutinho na beki Joao Pereira wote kwa pamoja wameposti picha za vyumba vyao kwenye mtandao wa Twita na Instagram wakifurahia kabla ya kucheza mchezo wao wa ufunguzi wa kundi D dhidi ya Ujerumani mjini Salvador juni 16.
Licha ya wasiwasi uliotanda juu ya Ronaldo kukivaa kikosi cha Joachim Low baada ya kusumbuliwa na majeruhi ya mguu aliyoipata kwenye mechi za UEFA, nyota huyo mwenye miaka 29 ameonekana kuimarika hasa baada ya kucheza kwa dakika 66 kwenye ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya Ireland siku ya jumatano.
Baada ya mechi ya Ujerumani, vijana wa Paulo Bento watakabiliana na Marekani juni 22 mjini Manaus, kabla ya kucheza mechi ya mwisho ya makundi mjini Brasilia dhidi ya Ghana juni 26.
Hoteli ya Argentina kwenye kombe la dunia ilipangwa mapema wiki hii, huku ikionesha wachezaji gani watakuwa wanalala chumba kimoja wakati wote wa mashindano.
Mpangilio unaonesha kuwa washambuliaji Messi na Aguero watakuwa wanalala chumba kimoja.

Anajisikia nyumbani: Joao Pereira pia aliposti picha hii inayomuonesha akicheza mpira (kulia)

Chumba kimoja: Orodha ya wachezaji wa Argentina watakaokuwa wanalala chumba kimoja wakati wa fainali za kombe la dunia.
0 comments:
Post a Comment