Wamemrudisha Wambura: Wa kwanza kutoka kulia ni
Mkurugenzi Msaidizi, Sheria na Wanachama TFF, Eliud Mvela, (Katikati) ni
mwenyekiti wa kamati ya rufani ya TFF, Wakili, Julius Mutabazi Lugaziya na ( watatu
kutoka kushoto) ni Juma Abeid Spencer, mjumbe wa kamati ya rufani wakati wa
mkutano na waandishi wa habari mchana huu.
Na Baraka Mpenja, Dar es
salaam
Imechapishwa Juni 11, 2014, saa 8:14 mchana
KAMATI ya rufani ya shirikisho la soka Tanzania, TFF, imetengeu maamuzi ya kamati ya uchaguzi
wa klabu ya Simba sc wa kuliengua jina la
mgombea wa Urais wa klabu hiyo, Micheal Richard Wambura.
Mwenyekiti wa kamati hiyo, wakili Julius Lugaziya
amesema mchana huu katika mkutano na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa
mikutano wa TFF, jijini Dar es salaam kuwa kamati yake ilikaa juzi na jana na
kufikia maamuzi ya kutengue maamuzi ya kamati ya uchaguzi ya Simba chini ya
mwanasheria, Dkt. Damas Ndumbaro kwasababu klabu hiyo ilikiuka kanuni ilijiwekea
yenyewe kwa mujibu wa katiba.
Lugaziya amesema kuwa uamuzi wa kumrudisha Wambura
umeangali zaidi busara kwasababu Simba ilikiuka katiba yake kwa kumuacha
mwanachama aliyesimamishwa kuendelea kufanya shughuli za klabu, na kama
akiondolewa basi katiba na kamati ya uchaguzi vyote vitakuwa batili.
“Tangu aliposimamishwa,
muomba rufani (Wambura) hajawahi
kuchukuliwa kama mtu aliyesimamishwa. Kwanini?, kupoteza haki za uanachama ni
pamoja na kupoteza haki za kulipa ada, haki za kushiriki mikutano, haki ya vikao
vya maamuzi na haki ya kuteuliwa katika vyomvyo mbalimbali vya Simba SC”. Alisema
Wakili Lugaziya.
“Tangu kutangazwa kusimamishwa, amekuwa akishiriki
shughuli za Simba”
“Amekuwa akishiriki mikutano yote mikuu na
dhararu, ikumbukwe kuwa mwanachama halali tu ndiye anatakiwa kushiriki mikutano
hiyo na mwanachama ambaye amesimamishwa hatakiwi kushiriki, lakini tangu
kutangaza kusimamishwa, Wambura amekuwa akishiriki”. Alifafanua Lugaziya.
“Kubwa zaidi, mpaka sasa Wambura ni mjumbe wa kuteuliwa
wa kamati ya utendaji ya Simba na alishiriki katika mikutano ya katiba pamoja
na kushiriki kuiteua kamati ya uchaguzi”.
Moto
kuwaka: Wambura dhidi ya Aveva ngoma nzito uchaguzi Simba sc, jamaa arudishwa
na kamati ya rufani.
Wakili huo aliongeza kuwa kama mtu batili
ameshiriki kufanya maamuzi, basi maamuzi nayo ni batili.
“Wambura alishiriki katika mkutano wa katiba na
kuiteua kamati ya uchaguzi, maana yake kama Wambura ni batili, basi katiba na
kamati ni batili”.
“kama tunafikia maamuzi ya kusema katiba na kamati
ya uchaguzi ya Simba si halali,
kwasababu mtu batili alishiriki, athari
yake ni kubwa. Kamati alishasema huko nyuma kwamba Simba ilikuwa inamchukulia Wambura
kama mwanachama”. Alisema Lugaziya.
“Naomba mnielewe kuwa uamuzi huu, hauna maana
nyingine au nia ya kutoa mlango kwa wanachama wa Simba au klabu nyingine kwenda
mahakamani, bali ni kwamba unawataka wanachama wa TFF kuzingatia na kufuata
taratibu walizojiwekea na si kutizumia kwa manufaa ya wachache katika mchezo wa
mpira wa miguu”.
“Kamati ya uchaguzi ya TFF inabatilisha uamuzi wa
kamati ya uchaguzi ya Simba. Michael Richard Wambura anastahili kugombea katika
uchaguzi huo”. Alimaliza Wakili Lugaziya.
Hata hivyo, Lugaziya alifafanua kuwa uamuzi
umefikiwa kwa wingi wa kura kwasababu maamuzi ya vikao kama hivyo kama wajumbe
wanashindwa kufikia muafaka maamuzi yanaamuriwa kwa kupiga kura.
Hii ni mwanzo, yapo mengi yamezungumzwa na mtandao
huu utakuletea habari zaidi. Endelea kuwa nasi.
0 comments:
Post a Comment