Wednesday, June 11, 2014



http://1.bp.blogspot.com/-3ToVu2drl3g/U1U_TqfMOnI/AAAAAAAADAc/XzB2-DLOjwQ/s1600/jj.JPG
Na Mwandishi Wetu, Tanga

Imechapishwa Juni 11, 2014, saa 10:54 jioni

KLABU ya Coastal Union inatarajiwa kufanya mkutano mkuu wa mwaka wa
wanachama utakaofanyika kwenye ukumbi wa Hotel ya Mkonge mkoani Tanga Juni 22 mwaka huu ambao utakuwa na agenda kuu mbili muhimu zitakazo jadiliwa na mengineyo.

Akizungumza jana,ofisa Habari wa timu ya Coastal Union,Oscar Assenga alisema kwenye mkutano huo utakuwa na agenda mbalimbali lakini ya  kwanza itakuwa ni kupokea taarifa na kujadili taarifa za kazi kutoka kamati mbalimbali za utendaji ndani ya klabu hiyo kwa kipindi kilichopita.

Assenga alisema pamoja na hayo lakini kutakuwa na kuthibitisha bajeti kwa mwaka wa fedha unaofuata baada ya mwaka uliopita kumalizika ambapo mkutano huo hautaruhusu wanachama wanaodaiwa madeni kuhudhuria.

Aidha alisema pia watafanya marekebisho ya katiba kwa kuongeza kifungu
cha kamati ya maadili ambapo hilo likiwa ni agizo la shirikisho la
soka hapa nchini kwa mujibu wa maelekezo kutoka shirikisho la soka
nchini.

       “Pia tutafanya marekebisho ya katiba kwani tutaongeza kifungu
cha kamati ya maadili ambacho ni muhimu ikiwa ni agizo la shirikisho
la soka nchini (TFF) “Alisema Assenga.

Hata hivyo aliwataka wanachama waliopo sehemu mbalimbali hapa nchini
kuhakikisha wanatimiza haki yao ya msingi kwa kuhudhuria kwenye
mkutano huo muhimu kwa ajili ya maendeleo ya timu hiyo kongwe hapa
nchini.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video