Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
TAARIFA zilizotufikia muda zinaeleza kuwa kikao
cha kamati ya Rufani ya shirikisho la soka Tanzania, TFF, kimemalizika
jioni hii na kuamua kuitupilia mbali
rufaa ya Michael Richard Wambura aliyekuwa anapinga kuondoshwa kwa mara ya pili
katika uchaguzi wa Simba.
Kwa maana kamati ya Wakili Lugaziya imeungana
rasmi na kamati ya uchaguzi ya Simba kuwa Wambura ana makosa kwa mujibu wa
kanuni za uchaguzi.
Wambura alikuwa mgombea wa nafasi ya Urais ambaye
jina lake lilienguliwa na kamati ya uchaguzi kwa mara ya kwanza na alikata
rufaa ambapo alishinda na kurejeshwa katika kinyang`anyiro hicho.
Lakini kamati ya uchaguzi ya Simba ilimuengua tena
baada ya kubainika amepiga kampeni kabla ya muda.
Wambura alipinga maamuzi hayo na kukata rufani ya
pili ambayo imesikilizwa leo na kamati ya Rufani ya uchaguzi ya TFF, lakini
ameangukia pua baada ya rufani yake kutupiliwa mbali.
Hata hivyo katika kikao hicho, mwenyekiti wa
kamati hiyo, Wakili Julius Mutabazi Lugaziya hakuweza kuhudhuria na imeelezwa
kuwa alibanwa na majukumu mengine ya kikazi.
Alipotafutwa Wakili Lugaziya amekiri kushindwa
kuhudhuria, lakini kwa mujibu wa sheria wajumbe wanne waliohudhuria walikuwa na
haki ya kuendelea na kikao na wamefanya hivyo.
Kabla ya kikao hicho, kulikuwa na shutuma juu ya
wakili Lugaziya kuwa anambeba Wambura, hivyo ameamua kususia kikao hicho ili
kukwepa lawama, lakini yeye ameeleza kuwa asingeweza kufanya hivyo kwasababu
yeye ni mwajiriwa wa TFF na anafanya kazi chini ya bosi wake, hivyo kutohudhuria
na kwasababu ya udhuru.
Lakini kuhusu kilichojiri, Lugaziya amesema
hajawasiliana na wajumbe wa kamati hiyo ili kujua maamuzi.
Mtandao huu unafuatilia taarifa rasmi kuhusu
jambo, lakini Wambura amesema anamwachia mungu ana atapigana kuona haki
inatendeka Simba.
0 comments:
Post a Comment