Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
0712461976
Imechapishwa Juni 10, 2014, saa 2:37 usiku
HATIMAYE
kamati ya rufani ya shirikisho la soka Tanzania, TFF imemaliza kujadili
rufani ya mgombea wa urais katika uchaguzi wa klabu ya Simba sc unaotarajia
kufanyika juni 29 mwaka huu, Michael Richard Wambura.
Kamati ya Rufani chini ya mwenyekiti
wake,wakili, Julius Luhaziya imekaa
kuanzia jana juni 9 mpaka jioni ya leo (juni 10) katika Hoteli ya Courtyard
iliyopo Upanga , jijini Dar es salaam.
Kikao hicho kilichojaa usiri mkubwa kimemalizika
jioni ya leo na kufikia maamuzi juu ya rufani ya Wambura, lakini mwenyekiti wa
kamati , Lugaziya ataongea na waandishi wa habari kesho mchana majira ya saa
6:00 katika ukumbi wa mikutano wa TFF.
Afisa habari wa shirikisho la soka Tanzania, TFF,
Boniface Wambura Mgoyo dakika chache zilizopita amesema kuwa kamati imeshamliza
na kufoloa maamuzi juu ya hatima ya Richard Wambura, lakini yeye hataki kuwa
msemaji wake kwani mwenyekiti atakuwa na mkutano na waandishi wa habari hapo
kesho mchana.
Wambura amefafanua kuwa kamati hiyo imekaa kwa
siku mbili kwasababu ndio chombo cha kutenda haki kwa pande zote, hivyo wajumbe
walikuwa wanapitia kwa umakini maelezo ya pande husika ili kufikia maamuzi
sahihi.
Mgombea Michael Wambura alikata rufani kupinga
kuondolewa katika mchakato wa uchaguzi wa Simba na kamati ya uchaguzi
inayoongozwa na wakili, Dkt. Damas Daniel Ndumbaro.
Sababu kubwa zilizokatiwa rufani kupinga Wambura
kugombea katika uchaguzi wa Simba ni
mbili ambazo ni kuipeleka Simba mahakamani
na kusimamishwa uanachama.
Taarifa za chini ya kapeti zimeshatoka, lakini si
misingi yetu ya kufanya kazi kwa kuandika taarifa zisizo rasmi.
Tusubiri mkutano wa kesho baina ya mwenyekiti wa
kamati ya Rufani na waandishi wa habari, hivyo wadau kuweni na subiri wakati
huu ambao mnataka taarifa juu ya suala.
Mbivu na mbichi zitafahamika kama kamati ya
Ndumbaro itashinda au Michael Richard Wambura.
Chukueni tahadhari juu ya taarifa zinazoendelea
kutolewa na mitandao mbalimbali ya kijamii juu ya Wambura kushinda au
kushindwa, jibu rasmi kutoka kwa wahusika halijatoka mpaka kesho mchana.
0 comments:
Post a Comment