Tuesday, June 3, 2014



 http://3.bp.blogspot.com/-pOkFUT6Np54/Uu-1U5fwroI/AAAAAAAABVo/R4wod4k4GAg/s1600/IMG_8383.JPG
Na Gervas Mwatebela, Dar es salaam

Imechapishwa Juni 3, 2014, saa 11:13 jioni

Baraza la sanaa Tanzania BASATA litaanza kuadhimisha siku ya msanii
Tanzania Oktoba 25 mwaka huu kwa kuenzi kazi mbalimbali zinazofanywa
na wasanii.
Taarifa iliyotolewa na BASATA kwa vyombo vya habari imefafanua kuwa
siku hiyo ya Oktoba 25 itaadhimishwa kitaifa katika mikoa mbalimbali
kutegemea na uwezo wa mikoa husika.

Sanaa ni kazi yoyote ambayo huusisha ubunifu katika uumbwaji wake na
Tanzania kama ilivyo kwa nchi nyingine imejaaliwa kuwa na vipaji vya
sanaa za aina mbalimbali zikiwemo muziki, uchoraji, filamu, ngoma za
asili, mitindo ya mavazi nakadhalika.

Kwa kuliona hilo baraza la Sanaa Tanzania BASATA limekuja na wazo la
kuadhimisha siku ya msanii Tanzania kila ifikapo Oktoba 25 kila mwaka.

Mkurugenzi wa maendeleo BASATA, Vivian Shaluwa amesema siku hiyo itaambatana na utoaji zawadi kwa wasanii ambao bado wanachipukia katika sanaa mbalimbali miongoni mwa hizo ni sinema bora, mpigaji vyombo bora wa muziki wa asili mbunifu wa mavazi na msanii chipukizi.

Baadhi ya wadau watakao shirikishwa katika siku ya msanii wa Tanzania,
ni pamoja na kampuni ya Haak Neel Production, ambapo hapa wanaeleza
kuguswa kwa wazo hilo.

Siku ya Msanii Tanzania itazinduliwa rasmi Juni sita mwaka huu jijini
Dar es Salaam ikiwa na kauli mbiu ya Sanaa ni Kazi ambapo Waziri wa
Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Daktari Fenella Mkangara anataraji
kuwa mgeni rasmi.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video