
Mshambuliaji wa Italia Mario Balotelli (kushoto) anatarajia kumuoa mpenzi wake Fanny Neguesha (kulia).
MSHAMBULIAJI
wa Italia, Mario Balotelli amemalizia maandalizi yake ya mwisho ya
kombe la dunia kwa kumchumbia rasmi mpenzi wake Fanny Neguesha wakati
huu akijiandaa kucheza mechi ya ufunguzi ya kombe la dunia jumamosi
dhidi ya England mjini
Manaus.
Mshambuliaji
huyo wa AC Milan ameposti picha ya mchumba wake mpya kwenye mtandao wa
Instagram siku ya jumatatu akiwa amevalia pete kidoleni.
Balotelli
aliisindikiza picha hiyo na maneno yaliyosema : `Alisema ndiyo`. Hii ni
ndiyo muhimu sana katika maisha yangu. Hiyo ndio ilikuwa sehemu ya
swali langu! nakupenda na sherehe njema ya kuzaliwa!
Uthibitisho: Balotelli aliposti picha hii ya Fanny akiwa amevalia pete ya uchumba kwenye mtandao wa Instagram
Balotelli aliposti picha hii kwenye mtandao wa Twita akiwa na mpenzi wake Fanny mapema mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment