Nahodha wa England, Steven Gerrard amemkosoa mwamuzi wa mechi yao yao ya jana waliyotoka suluhu.
NAHODHA
wa England, Steven Gerrard amesikitishwa na kiwango kibovu cha mwamuzi
katika suluhu waliyoipata jana dhidi ya Honduras ikiwa ni mechi ya
kulipashia kombe la dunia mjini Miami.
Pia Gerrard amewalaumu wapinzani wao kwa mchezo mbovu ambapo
wachezaji wanne walioneshwa kadi za njano na Brayan Beckeles alitolewa
nje kwa kadi nyekundu baada ya kumfanyia madhambi Leighton Baines na hii
ilitokana na kupata kadi mbili za njano.Hata
hivyo mechi hiyo ilisimama kwa nusu saa kutokana na umeme kukatika
uwanjani, lakini haikupunguza kasi ya Honduras walioonesha kuwa hatari
katika mechi hiyo.
Gerrard amemkosa mwamuzi Salazar na wachezaji wa Honduras baada ya mechi.
“Tulikuwa
na mawazo kwenye vyumba vya kubadilishia nguo”, aliwaambia waandishi wa
habari. “Tulifikiri kuwa mwamuzi alikuwa mbovu. Lakini tumefurahi
kwasababu hatujapa majeruhi yeyote”.
“Walikuwa
wanacheza vibaya wakati wanajua imebaki wiki tu kuanza kombe la dunia.
Nashangaa sana inapotokea mchezaji anacheza mpira kifuani kwa mchezaji,
ile ni kadi nyekundu. Ilitokea kipindi cha kwanza na pengine ingebadili
mpira”
0 comments:
Post a Comment