Na Baraka Mpenja, Dar
es salaam
WAGOMBEA wawili , Evans
Eliez Aveva na Andrew Peter Tupa wamepitishwa kugombea Urais wa klabu ya Simba
katika uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika juni 29 mwaka huu, jijini Dar es
salaam.
Akizungumza leo mchana
na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano wa shirikisho la soka la
Tanzania, TFF, mtaa wa Ohio, Posta, jijini Dar es salaam, Mwenyekiti wa kamati
ya uchaguzi, Wakili Dkt. Damas Daniel Ndumbaro alisema wagombea wote
waliopitishwa ni sasa ruksa kuanza kampeni.
Hata hivyo kampeni hizo
lazima ziwe za ustaarabu, heshima na kutotumia lugha ya matusi.
Aidha, Wakili Ndumbaro
aliwataja wagombea wanne katika nafasi ya umakamu wa Rais ambao ni Geofrey
Nyange Kaburu, Jamhuri Musa Kiwhelo `Julio`, Bundala Kabulwa na Swedi Nkwabi.
Nafasi za ujumbe wa
kamati ya utendaji upande wa wanaume watu 18 wamevuka kigingi ambao ni Yasini
Mwete, Ally Suru, Said Tully, Rodney Chiduo, Said Pamba, Ally Chaurembo,
Abdulhamid Mshangama, Chano Almasi, Damian Manembe, Ibrahim Masoud, Kajuna
Noor, Hamisi Mkoma, Alfred Elia, Saidi Kubenea, Idd Mkamballah, Juma Mussa,
Maulid Abdallah na Collin Frisch.
Kwa upande wa wanawake wamepitishwa watu watatu ambao ni Asha
Muhaji, Jasmine Badour na Amina Poyo.
Uchaguzi wa Simba kwa
muda mrefu umegubikwa na mizengwe iliyotokana na kuenguliwa kwa jina la mgombea
wa Urais, Michael Richard Wambura.
Baada ya kuenguliwa,
Wambura alikata Rufaa katika kamati ya Rufani ya uchaguzi ya TFF chini ya
mwenyekiti, Wakili Julius Mutabazi Lugaziya akipinga kuenguliwa kwa jina lake
na baadaye alishinda.
Lakini aliondoshwa kwa
mara ya pili kwa kupiga kampeni kabla ya muda.
Hata hivyo kuna taarifa
kuwa baadhi ya wanachama wanamuunga mkono Wambura wameshatua mahakani wakitaka mahakama isimamishe uchaguzi
uliopangwa kufanyika juni 29.
Wanachama hao
wanaosemekana kuwa wafuasi wa Wambura wanadai kamati ya uchaguzi na kamati ya
rufani ya TFF haikumtendea haki Wambura, hivyo wanaiomba mahakama isimamishe
uchaguzi huo.
0 comments:
Post a Comment