
Bluu: Cesc Fabregas amesaini mkataba wa miaka mitano katika klabu ya Chelsea akitokea Barcelona.
KLABU ya Arsenal atapata paundi milioni 5.6 katika mauzo ya mchezaji wake wa zamani Cesc Fabregas kutoka klabu ya Bracelona kwenda Chelsea.
Kiungo
huyo wa Hispania amekamilisha usajili wake na kurudi London jana
alhamisi kwa dau la paundi milioni 30 akitokea Barcelona na amesaini
mkataba wa miaka mitano utakaompatia mshahara wa paundi laki moja na
nusu kwa wiki.
Lakini
biashara hiyo pia itainufaisha Asernal na kuongezea fedha hizo katika
paundi milioni 100 zilizotengwa katika usajili na zitawasaidia sana
kumnunua Mario Balotelli ambaye ni chaguo la kwanza la kocha Arsene
Wenger majira ya kiangazi mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment