Friday, May 2, 2014



ZLATAN Ibrahimovic ametangaza kumalizia soka lake katika klabu yake ya Paris Saint-Germain.
Nyota huyo mwenye miaka 32 kwa sasa alijiunga na PSG majira ya kiangazi mwaka 2012 na sasa amebakiwa na miaka miwili katika mkataba wake na amekanusha taarifa za kuhusishwa kuondoka Parc Des Princes.
Akizungumza na jarida za PSG, Ibrahimovic alisema: “wakati mwingine unasoma kwenye magazeti, au sehemu yoyote, unasikia tetesi za uwezekano wa kuondoka”.
“Kwahiyo nasema wazi: nina furaha kuwepo Paris na sina nia ya kumalizia soka langu sehemu nyingine zaidi ya hapa Paris”.
Wakiwa mbele kwa pointi 8 katika msimamo wa Ligue 1, PSG wana uwezo mkubwa wa kutwaa kwa mara ya pili mfufulizo endapo watashinda jumamosi dhidi ya Sochaux.
Ibrahimovic ambaye hajacheza tangu alipopata majeruhi ya nyama za paja kwenye mchezo wa kwanza wa robo fainali ya UEFA dhidi ya Chelsea anatarajia kuwasaidia vijana wa Laurent Blanc kumalizia kibarua mei 7 mwaka huu dhidi ya Rennes.
Aliongeza: “Tutakuwa na nafasi nyingine ya kushinda taji mchezo ujao. Natumaini kucheza. Kama ikitokea hivyo, naweza kusema, nina uhakikisha tutabeba kombe tena na tutashangilia ushindi siku hiyo”.
Mpaka sasa, Ibrahimovic ndiye anayeongoza kufunga mabao mengi Ligue 1 ambapo mpaka sasa ametia kambani mabao 25.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video