ZINEDINE
Zidane amekanusha tetesi kuwa anataka kuondoka Real Madrid mwishoni mwa msimu
huu kwa lengo la kuanza kazi yake ya kwanza akiwa kocha mkuu.
Nyota
huyo wa zamani wa Ufaransa kwasasa ni msaidizi wa Carlo Ancelotti, Santiago
Bernabeu baada ya kucheza kwa mafanikio makubwa na kushinda kombe la dunia,
kombe la ulaya, UEFA na makombe mawili ya ligi akiwa kwao ufaransa na Hispania.
Zidane
amekuwa akihusishwa sana kurudi nyumbani kwao wiki za karibuni, huku klabu zake
za zamani za Monaco na Bordeaux zikionesha nia ya kumpatia kazi.
Zidane
mwenye miaka 41 kwasasa amesisitiza kuwa hana mawasiliano yoyote na klabu hizo
mbili.
“Kama
kawaida, kila mtu anazungumza yake,” Zidane amewaambia L`Equipe. “na siku zote nalazimishwa kujibu hili”.
“Sina
mawasiliano, hata ya siri na Monako kama ninavyosikia. Kwa kifupi, sijawahi
kuwasiliana na mtu yeyote”.
“Nipo
chini ya mkataba na Real Madrid, niko na Real na macho yangu yapo kwa Real,
naangalia ligi kuu na ligi ya mabinngwa. Nukta!”.
0 comments:
Post a Comment