Sunday, May 18, 2014


Zidane tips France for strong World Cup campaign

LEJENDARI wa Ufaransa, Zinedine Zidane anaamini timu ya taifa ya nchi hiyo itafanya maajabu katika fainali za mwaka huu za kombe la dunia nchini Brazil kuanzia juni 12 hadi juni 13.
Kikosi cha kocha Didier Deschamps kwa asilimia zote kilishindwa kufuzu fainali za kombe la dunia, lakini kilifanya maajabu katika mechi mbili za mtoano dhidi ya Ukraine.
Zidane anaamini Karim Benzema na Frank Ribery ni wachezaji watakaoisaidia Ufaransa kutafuta ubingwa.
“Ufaransa itafanya vizuri, “ kocha huyo msaidizi wa Real Madrid amewaambia The times of India.
“Mara ya mwisho nchini Afrika kusini walimvunja moyo kila mtu, lakini kwasasa chini ya Didier Deschamps wanacheza vizuri”.
Ufaransa inaokana kuwa na nafasi ya kufuzu hatua ya makunndi ya kombe la dunia baada ya kupangwa na nchi zinazoonekana dhaifu ambazo ni Switzerland, Ecuador na Honduras.
Hata hivyo Zidane amewaonya wacheza wa Ufaransa kutodharau mechi za mwanzoni  kwani wanaweza kujikuta wanapanda ndege mapema.
Aliendelea: “ uko pale kwasababu ni miongoni mwa nchi 32 bora kwa soka duniani”.
“Katika kundi E hakuna timu yoyote inayotoka Ulaya ukiitoa Ufaransa. Kwa asilimia kubwa hawajui mpira wetu na watacheza kwa staili ya bara lao. Sio kundi rahisi hata kidogo”.
Wachambuzi wengi wa soka wanawapa nafasi Brazil na Argentina kutwaa kombe la mwaka huu kutokana na kuchezwa katika ardhi yao ambayo hakuna taifa la Ulaya lililowahi kubeba kombe.
Lakini Zidane amekataa mawazo hayo na kuamini kuwa Ufaransa, Ujerumani na Hispania ni nchi  zinazoweza kutwaa ubingwa mwaka huu.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video