Klabu
ya Young Africans imeeingia makubaliano na Benki ya Posta nchini juu ya
mabadiliko ya utengenezaji wa kadi za wanachama kutoka kwenye mfumo wa
zamani (analogy) kwenda kwenye mfumo mpya wa kisasa (digital) ambapo
sasa wanachama wake watakua wakitumia kadi zenye mfumo wa ATM.
Mkurugenzi Masoko wa Benki ya Posta nchini
Bw. Deo Kwiyukwa amesema wamefikia makubaliano hayo baada ya kukaa na
viongozi na kuona njia hiyo itaisaidia klabu kuongeza mapatao kwani wigo
wake wa kuandikisha wanachama utakua ni mkubwa kwa nchi nzima na kwa
muda mfupi.
"Badala ya wanachama kuja
Dar es salaam makao makuu kujaza fomu za uanachama watakua wanaweza
kufanya hivyo popote walipo kwa kwenda ofisi za Benki ya Posta na kujaza
fomu hizo na baadae kupewa kadi ya uanachama" alisema Deo.
Gharama
za kujiunga na uanchama zitabakia zile zile Tshs 15,000/=, na ada ya
mwaka elfu Tshs 12,000/= ambapo mwanachama wa Yanga atapata kadi ya TPB
yenye logo ya timu yake ambayo pia ataitumia kwenye shughuli za kibenkI
kwa huduma ya kuweka na kutoa fedha.
Naye
Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga Clement Sanga amesema anaishukuru
Benki ya Posta kwa kuweza kufikia makubalianao hayo, kwa kutumia mfumo
huu wa kisasa tutaweza kujua idadi ya wachama wetu walio hai kwa wepesi
zaidi na taarifa zetu zitaweza kuwafikia wanachama kwa uharaka zaidi.
Uzinduzi
rasmi wa kadi mpaya za uanachama utafanyika tarehe 16.05.2014 kwenye
hoteli ya Hyatt Kempsinki eneo la Posta (zamani Kilimanjaro Hotel) na
mara baada ya uzinduzi moja kwa moja zoezi la kuhamisha wanachama kutoka
kwenye mfumo wa analogy kwenda digital utaanza.
0 comments:
Post a Comment