WAKALA wa Mario Balotelli ameweka wazi kuwa
amepokea taarifa kutoka kwa mkurugenzi wa AC Milan, Adriano Galliani kuwa nyota
huyo hatauzwa majira ya kiangazi mwaka huu.
Mshambuliaji huyo raia wa Italia ndiye mfungaji
bora wa klabu hiyo msimu huu akiwa ametia kambani mabao 14 katika mechi zame 28
za Seria A alizocheza.
Lakini hatima yake haijulikani hasa baada ya
kupondwa sana kufuatia kufanya vibaya katika mechi waliyofungwa na Roma, huku
nyotq huyo akimuwakia vikali kocha wake Clarence Seedorf kwa kumtoa uwanja, pia
aliwakemea vilai watangazaji wa Sky sports waliokuwa wanamponda baada ya mechi.
“(Milan) wameniambia Mario Balotelli hauzwi
japokuwa tutasikia tetesi nyingi,” wakala huyo amewaeleza Calciomercato.com.
“Adriano Galliani aliniambia hauzwi na hili
limenipa furaha kubwa”.
‘Kutoka muda huu mpaka
agosti 31 tutasikia tetesi nyingi kuhusu hatima yake, lakini hilo sio tatizo”.
0 comments:
Post a Comment