
RUUD
van Nistelrooy ameshangazwa na ofa aliyopewa na Guus Hiddink kuwa kocha wake
msaidizi atakapoanza majukumu ya kukinoa kikosi cha timu ya taifa ya Uholanzi baada ya
kumalizika fainali za kombe la dunia mwaka huu nchini Brazil.
Bosi
wa sasa Louis Van Gaal anatarajia kuachia nafasi hiyo baada ya kombe la dunia
baadaye mwaka huu, na Hiddink anatarajiwa kurithi mikoba yake na kuiongoza
Uholanzi kufuzu fainali za kombe la Ulaya mwaka 2016.
Hiddink
aliyewahi kufanya kazi katika klabu za Real Madrid na Chelsea, pamoja na timu
za taifa za Russia, Australia na Korea
kusini amemuomba Van Nistelrooy kuungana naye na kuwa kocha msaidizi.
Mshambuliaji
huyo wa zamani aliyefunga mabao 35 katika mechi 70 za timu yake ya taifa
amekiri kuwa ofa hiyo imemshitua sana.
“Ilikuwa
ni mshangao kupokea simu ya Hiddink,” ameuambia mtandao wa Uefa.com. “Kiukweli
sikutegemea kitu kama kile, lakini kazi kama hii inapokuja ni heshima.
“Kufanya
kazi na Hiddink mwenye uzoefu mkubwa wakati kwangu mimi ndio kwanza naanza kazi
ya ukocha, ni ajabu”.
Van
Nistelrooy aliongeza kuwa ana matumaini ya kusaidia soka la taifa.
“Nitakuwa
kocha msaidizi, kwahiyo nitamsaidia kila mtu pamoja na kocha mwingine msaidizi
Danny Blind”, Aliongeza.
“Ninaweza kutumia uzoefu
wangu kuonesha namna ya kukabiliana na presha, nitaonesha namna nilivyokuwa
nafanya vitu na hali iliyokuwa inanitokea-lakini ni vitu vikubwa ambavyo naweza
kumfundisha kila mchezaji”.
0 comments:
Post a Comment