KOCHA
wa timu ya Taifa ya Ujeruman, Joachim Law ametaja kikosi cha awali cha
wanandinga 30 kwa ajili ya kombe la dunia majira ya kiangazi mwaka huu nchini
Brazil, huku mshambuliaji wa Fiorentina, Mario Gomes akiachwa.
Nyota
huyo wa zamani wa Bayern Municha amekuwa akisumbuliwa na majeruhi msimu huu na
badala yake Low amemuita mshambuliaji kinda wa Hoffenheim, Kevin Volland.
Kipa
wa Borussia Monchengladbach, Marc-Andre
ter Stegen anayehusishwa kujiunga na
Barcelona majira ya kiangazi mwaka huu naye akiachwa, huku Ron-Robert Zieler
akichukuliwa kama mlinda mlango namba tatu.
Wakati
huo huo, kiungo wa Real Madrid, Sami Khedira amejumuishwa katika kikosi hicho
licha ya kukosa mechi nyingi kwasababu ya majeruhi.
Mbali
na Volland, vijana wengi kama vile Erik Durm, Shkodran Mustafi, Matthias
Ginter, Leon Goretzka na Max Meyer ni miongoni mwa wachezaji waliojumuisha
katika kikosi hiki ambacho kitachujwa na kufikia wachezaji 23 ambao watatajwa
juni 2 mwaka huu tayari kwa kuelekea Brazil.
Ujerumani
watakutana na Ureno, Ghana na Marekani hatua ya makundi ya kombe la dunia.
KIKOSI KAMALI HIKI HAPA:
Walinda mlango :
Manuel Neuer (Bayern Munich), Roman Weidenfeller (Borussia Dortmund), Ron-Robert
Zieler (Hannover)
Walinzi : Jerome
Boateng (Bayern Munich), Erik Durm (Borussia Dortmund), Kevin Grosskreutz
(Borussia Dortmund), Benedikt Howedes (Schalke), Mats Hummels (Borussia
Dortmund), Marcell Jansen (Hamburg), Philipp Lahm (Bayern Munich), Per
Mertesacker (Arsenal), Shkodran Mustafi (Sampdoria), Marcel Schmelzer (Borussia
Dortmund)
Viungo : Lars Bender
(Bayer Leverkusen), Julian Draxler (Schalke), Matthias Ginter (Freiburg), Leon
Goretzka (Schalke), Mario Gotze (Bayern Munich), Andre Hahn (Augsburg), Sami
Khedira (Real Madrid), Toni Kroos (Bayern Munich), Max Meyer (Schalke), Mesut
Ozil (Arsenal), Bastian Schweinsteiger (Bayern Munich)
Washambuliaji :
Miroslav Klose (Lazio), Kevin Volland (Hoffenheim), Lukas Podolski (Arsenal),
Marco Reus (Borussia Dortmund), Andre Schurrle (Chelsea), Thomas Muller (Bayern
Munich)
0 comments:
Post a Comment