Saturday, May 3, 2014



 Athletic Bilbao seal Champions League return with resounding win over Rayo
KLABU ya Atletic Bilbao amefufua matumaini ya kucheza ligi ya mabingwa barani ulaya msimu ujao baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Rayo Vallecano katika mchezo wa ligi kuu nchini Hispania, La Liga usiku huu.

Bilbao chini ya kocha Ernesto Valverde wameshinda dhidi ya wenyeji wao waliopo nafasi ya katikati ya msimamo na wameongeza nguvu ya kufuzu UEFA kwa mara ya kwanza tangu walipomaliza katika nafasi ya pili katika msimu wa La Liga msimu wa 1997-98.
Wiki iliyopita Bilbao walipata  ushindi mwingine wa mabao 3-1 dhidi ya Sevilla.
Mabao ya kipindi cha kwanza ya Mikel San Jose dakika ya 20 na Oscar de Marcos katika dakika ya 30 yalionesha upepo mzuri kwa Atletico Bilbao wenye `Mzuka` mkubwa wa kuonja uhondo wa UEFA mwakani.
Mabao hayo mawili yalisababishwa na kona mbili zilizochongwa kutoka winga ya kushoto na mabeki wa Vallecano kushindwa kuokoa.
Baada ya bao la De Marcos , mashabiki wa Bilbao waliingia karibu na uwanja wakiwasalimia wachezaji na kusababisha hofu ya kukosekana kwa usalama.
Lakini hakuna aliyepata matatizo na morali ya mashabiki wa Bilbao iliongezeka zaidi kipindi cha pili baada ya Ander Herrera kufunga bao katika dakika ya 74 kwa mpira wa adhabu ndogo.
Matokoe hayo yanaifanya Bilbao kuwa mbele kwa pointi 9 dhidi ya timu ya Sevilla iliyopo nafasi ya tano, huku ikiwa na mechi tatu, lakini haiwezi kuiondoa Bilbao katika nafasi hiyo kutokana na kuwa dhaifu msimu huu.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video