UBELGIJI
inatarajia kujipima nguvu dhidi ya timu ya Taifa ya Marekani kujiandaa na
fainali za FIFA za kombe la dunia zinazoanza kutimua vumbi juni 12 mpaka julai
13 mwaka huu.
Mechi
hiyo itachezwa karibu na mji wa Sao Paulo.
“Itakuwa
kama mechi ya mazoezi kwa kila timu”, chama cha soka nchini Ubelgiji kimesema
leo ijumaa.
Marekani
waliopo kundi G na timu za Ureno, Ujerumani
na Ghana.
Wataanza
kampeni za kombe la dunia juni 16 mwaka huu dhidi ya wawakilishi wa Afrika, timu
ya Taifa ya Ghana.
Ubelgiji
wataanza kampeni yao juni 17 dhidi ya wawakilishi wengine wa Afrika, timu ya
Taifa ya Algeria, baadaye watacheza na Russia na Jamhuri ya Korea katika mechi
za kundi H.
0 comments:
Post a Comment