Dar es Salaam. Bendi ya muziki wa dansi
ya The African Stars ‘wana twanga pepeta’ ijumaa itazindua ukumbi wa kisasa wa
burudani na mikutano wa Machinga Lounge uliopo maeneo ya uwanja wa mpira wa wa
miguu wa Karume jijini.
Ukumbi huo unamilikiwa na kampuni ya
African Stars Entertainment Tanzania (ASET), umetengenezwa kisasa
zaidi kwa lengo la kuwapa burudani mashabiki wa Manispaa ya Ilala, Temeke na
Kinondoni kwa mujibu wa mkurugenzi wa Twanga Pepeta, Asha Baraka.
Asha alisema kuwa kwa muda mrefu sasa
wakazi wa maeneo ya Ilala hawana ukumbi mkubwa kwa ajili ya shughuli za
burudani na yeye kuamua kutengeneza ukumbi huo uliopo eneo maarufu la Machinga
Complex.
“Hii ni fursa pekee kwa wadau wa
burudani kuzindua ukumbi huo ambao ni wa kisasa, lengo ni kuwapa burudani
mashabiki wetu wa maeneo hayo na majirani zake, hasa kwenye ukumbi wa kisasa
ambao hata shuguli za mikutano mbali mbali inaweza kufanyika,” alisema Asha.
Alisema kuwa ukumbi huo unauwezo wa
kuingiza watu zaidi ya 500 waliokaa kwenye viti na lengo lao kubwa pia kutumika
kwa vikundi vingine vya burudani. “Twanga haitakuwa inafanya shoo zake mara kwa
mara kwenye ukumbi huu, vikundi vingine, anamuziki wa bongo fleva na taarabu
pia wanakaribishwa, kuutumia,” alisema.
Hii ni mara ya pili kwa ASET kumiliki
ukumbi ambapo mwanzoni mwa miaka ya 2000 walimiliki ukumbi wa ASET Club (zamani
FM Club au Lang’ata) uliopo eneo la Kinondoni,
0 comments:
Post a Comment