Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
MABINGWA wa ligi kuu soka Tanzania bara, Azam fc
ndani ya siku mbili wamefanya usajili wa wachezaji wawili kutoka klabu ya Yanga
SC ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mapendekezo ya kocha mkuu, Mcameroon,
Joseph Marius Omog.
Juzi walifanikiwa kumsainisha aliyekuwa
mshambuliaji wa Yanga, Mrundi Didier Kavumbagu kwa mkataba wa mwaka mmoja, huku
kipengele cha kuongezewa mwaka mwingine kikiwepo kulingana na uwezo
atakaouonesha.
Wakati wapenzi wa soka wakijadiliana usajili wa
Kavumbagu, jana wengi walishituliwa na usajili mwingine mkubwa wa kiungo mahiri wa ukabaji wa Yanga, Frank
Domayo `Chumvi”.
Domayo alisaini Mkataba wa miaka miwili kuitumia
klabu ya Azam, huku taarifa zikieleza kuwa mkataba wake na Yanga ulikuwa
umemalizika mwishoni mwa msimu uliopita.
Usajili wa Domayo ulifanyika jana katika kambi ya
timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars iliyopo Tukuyu jijini Mbeya kwa
maandalizi ya mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Malawi mei 4 mwaka huu
uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Stars ipo katika mipango ya mchezo huo na
wachezaji wote wanaufikiria, lakini kwa Domayo imekuwa tofauti ambapo akiwa
huko ameamua kusaini Azam fc.
Ukirejea nyuma sio mara ya kwanza mchezaji kusaini
akiwa katika kambi ya timu ya taifa ya Tanzania.
Kelvin Yondani wakati anasaini Yanga kutokea Simba
alikuwa kwenye kambi ya Taifa stars.
Ilielezwa kuwa alitoroshwa na kiungozi mmoja
kwenda kusaini Yanga.
Kitendo kile kilitafsiriwa kuwa utovu wa nidhamu,
lakini baadaye suala hilo lilizimwa kiaina kwasababu ni utamaduni wetu.
Domayo si mara yake ya kwanza, kwasababu miaka
miwili iliyopita wakati akijiunga na Yanga kutoka JKT Ruvu alisaini mkataba
wake akiwa kambi ya Stars.
Baada ya usajili huo kukamilika, Katibu wa Azam
FC, Nassor Idrisa Mohamed ‘Father’ amekaririwa na Tovuti ya Azam akisema katika
kuendelea kukiimarisha kikosi chao kwa ajili ya msimu ujao wamepiga hatua
nyingine kwa kumsaini Domayo.
“Kama unavyojua, baada ya kumaliza msimu vizuri tukiwa mabingwa wa Bara, tuligundua mapungufu kwenye kikosi chetu na kwa ushauri wa mwalimu wetu (Joseph Marius Omog) ndiyo tunayafanyia kazi,”alisema Father.
Domayo anakuwa mchezaji wa wa pili ndani ya siku mbili kusajiliwa na Azam FC kutoka mabingwa wa zamani na mabingwa wa kihistoria Tanzania Bara, Yanga SC baada ya jana klabu hiyo kumsaini mshambuliaji Mrundi Didier Kavumbangu.
“Kama unavyojua, baada ya kumaliza msimu vizuri tukiwa mabingwa wa Bara, tuligundua mapungufu kwenye kikosi chetu na kwa ushauri wa mwalimu wetu (Joseph Marius Omog) ndiyo tunayafanyia kazi,”alisema Father.
Domayo anakuwa mchezaji wa wa pili ndani ya siku mbili kusajiliwa na Azam FC kutoka mabingwa wa zamani na mabingwa wa kihistoria Tanzania Bara, Yanga SC baada ya jana klabu hiyo kumsaini mshambuliaji Mrundi Didier Kavumbangu.
Kufautai usajili wa aina hiyo kujitokeza tena
katika kambi ya Taifa stars, shirikisho la soka Tanzania, TFF limeshituka na
kuanza taratibu za kuchunguza suala hilo linaloihusisha Azam fc na mchezaji
Frank Domayo akiwa kambini.
Taarifa iliyotumwa na afisa habari wa TFF asubuhi
hii inasema kuwa: “Kutokana na tukio lililotokea jana (Aprili 30 mwaka huu)
kwenye kambi ya timu ya Taifa (Taifa Stars) iliyopo Tukuyu mkoani Mbeya
likihusisha usajili wa baadhi ya timu, Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amemteua Wakili Wilson Ogunde kuchunguza mlolongo
mzima wa tukio hilo.
Baada ya kukamilisha uchunguzi wake, Wakili Ogunde
ataishauri TFF kuhusu hatua za kisheria na kikanuni za kuchukua.
TFF inatoa wito kwa wachezaji, klabu na wadau wa
mpira wa miguu kufuata kanuni na taratibu katika utendaji wao”.
0 comments:
Post a Comment