Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
MSHAMBULIAJI wa Yanga SC, Jeryson John Tegete
amesema kuwa ataendelea kuitumikia klabu hiyo msimu mpya wa ligi kuu soka
Tanzania bara.
Katika mahojiano maalumu na mtandao huu, Tegete
ameeleza kuwa hata itokeo klabu yoyote yenye dau nono kiasi gani hang`atuki Yanga sc.
Mshambuliaji huyo aliendelea kwa kusema Yanga
ilistahili kutwaa ubingwa msimu uliopita, lakini waliathiriwa na matokeo mabaya
katika mechi muhimu za mwisho, hivyo kwa nafasi yake anatarajia kuisaidia
kurejesha taji msimu ujao.
“Mechi za mwisho nilipata nafasi ya kucheza na
nilijisikia vizuri”.
“Muda mwingi nilikuwa sichezi na sikulalamika
kwasababu nilikuwa na majeruhi ya goti”.
“Mwisho mwisho nilikuja kucheza kwasababu
nilipona. Sahizi niko fiti na msimu ujao
nitacheza kwa amani sana kwasababu nimepona goti”. Alisema Tegete.
Tegete aliongeza kuwa bado ana mkataba na Yanga na
hana mpango wa kuhama kwasasa kwasababu anajiona kuwa na deni kufuatia
kutofanya vivuri kwa misimi miwili mitatu.
Mshambuliaji huyo kipenzi wa Wanajangwani
aliendelea kueleza kuwa licha ya kuwa na deni na Yanga, bado anaota kuitumikia
kwa mara nyingine timu ya taifa ya
Tanzania, Taifa Stars.
“Taifa stars mbona nitarudi! Aaah! Nimepona goti,
lazima nirudi kuonesha vitu vyangu”. Alisema Tegete kwa furaha.
Tegete pia amezungumzia kuondoka kwa wachezaji
wawili wa Yanga, Frank Domayo na Didier Kavumbagu kwenda Azam fc, ambapo amekiri
kuwa walikuwa muhimu, lakini hakuna haja ya kuwalilia kwasababu wapo wachezaji
wengine watakaopata nafasi ya kucheza.
‘Kweli walikuwa wachezaji muhimu, lakini kuondoka
kwao sio kwamba ni pengo kubwa mno”
“Wapo wachezaji wengine watakaopata nafasi. Akina
Telela walikuwa hawachezi, sasa utakuwa wakati wao”.
“Mpira ndivyo ulivyo, kuondoka ni kawaida.
Mashabiki wasiumize kichwa na kushindwa kulala, watu wengine wapo”.
“Mpira ni kupata nafasi ili uoneshe uwezo. Sasa
wengine wakipata nafasi wataonekena”.
“Wao walipata nafasi ndio maana walionekana.
Itakuwa nafasi kwa wengine pia”.
“Tusahau yaliyopita tuganye yajayo, watu wasianze
kuwalaumu viongozi sana, kawaida tu”. Aliongeza Tegete.
Tegete kwa misimu miwili mfululizo ameshindwa
kuonesha makali yake kama miaka ya nyuma, lakini mwishoni mwa msimu uliopita
alipata nafasi ya kucheza baada ya kupona majeruhi yake ya goti.
Alifanya kazi nzuri kwa kushirikiana na Hussein
Javu ambaye naye alipata nafasi mechi za mwisho.
Kwa takribani msimu mzima uliomalizika aprili 19
mwaka huu, Mrundi Didier Kavumbagu alikuwa akicheza nafasi ya mshambuliaji wa
kati, lakini kwa sasa ameondoka na pengine inaweza kuwa nafasi nzuri kwa Tegete
msimu ujao.
0 comments:
Post a Comment