Na Baraka Mpenja, Dar es Salaam
KOCHA mpya wa Taifa Stars, Mart Nooij anatarajia
kuiongoza timu hiyo kwa mara ya kwanza katika mechi ya kirafiki ya kimataifa
dhidi ya timu ya taifa ya Malawi kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya leo jioni.
Hiki ni kipimo kizuri cha Nooij kujua makali ya
kikosi chake ambacho kiliweka kambi tangu aprili 27 mwaka huu, mjini Tukuyu kujiandaa na mchezo huo ikiwa ni
harakati za kujiweka sawa kabla ya kuanza kusaka tiketi ya kushirki kombe la
mataifa ya Afrika mwakani nchini Morocco.
Stars yenye mchanganyiko wa wachezaji wakongwe na
wale waliopatikana katika mpango wa maboresho ya Taifa stars wana jukumu kubwa
la kuwaaminisha watanzania kuwa watafuzu AFCON mwakani.
Mechi iliyopita ya kirafiki, Aprili 26 mwaka huu
walichapwa mabao 3-0 na akina Didier Kavumbagu, Amisi Tambwe na Yusuf Ndikumana
wa Burundi.
Huo ulikuwa mchezo maalum wa kuadhimisha miaka 50 ya muungano wa
Tanganyika na Zanzibara ambapo timu ya taifa ya Burundi iliizidi kwa kila kitu
Taifa stars iliyosheheni wachezaji wengi kutoka kikosi cha maboresho.
Kwa mara ya kwanza katika historia ya soka, uwanja
wa Sokoine utatumika kwa mechi ya Taifa stars.
Wapenzi wengi wa soka mkoani Mbeya wamefurahishwa
na maamuzi ya TFF kuipeleka mechi hii mkoani humo.
Hii imetokana na jitihada kubwa ya viongozi wa
chama cha soka mkoani Mbeya, MREFA na wamiliki wa uwanja wa Sokoine, CCM katika
kuuboresha uwanja na kuwa na hadhi ya
mechi ta Taifa stars dhidi ya Malawi.
Uongozi wa MREFA umewaomba wapenzi wa soka jijini
Mbeya kujitokeza kwa wingi kuishangilia Taifa stars leo hii ili kuwaaminisha
watanzania kuwa Mbeya ni mji uliojaa wapenda soka.
Kwa miaka mingi Stars imekuwa ikicheza zaidi Shk.
Amri Abeid, Arusha, CCM Kirumba, Mwanza, na shamba la bibi au Taifa, jijini Dar
es saala, lakini safari hii imekuwa zamu ya sokoine.
Mwenyekiti wa MREFA, Elias Mwanja ameuambia
mtandao huu kuwa maandalizi yote yamekamilika na hali ya hewa ni nzuri, hivyo
kinachosubiriwa kwa sasa ni muda kufika.
“Nawaombe mashabi wa soka jijini Mbeya kujitokeza
kwa wingi ili kuishangali timu yao ya Taifa”.
“Hii ni fursa adimu mno, wasiwaangushe watanzania
wenzao. Kwapamoja twendeni tukaishangilie timu yetu kwa moyo mmoja”. Alisema
Mwanjala.
Kiingilio katika mechi hiyo ya kimataifa ni
shilingi elfu tano tu (Tsh 5,000/=.
0 comments:
Post a Comment