Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
KWA
niaba ya wachezaji wenzake, mlinda mlango namba moja na nahodha wa timu ya
taifa ya Tanzania chini ya miaka 20, Ngorongoro Heroes, Aishi Manula
amekaririwa na mtandao huu akiwaomba wapenzi wa soka kujitokeza kwa wingi
kuwaunga mkono katika Mechi ya kwanza ya raundi ya pili ya michuano ya Afrika
kwa vijana wenye umri chini ya miaka 20.
Haya
ni maneno ya vijana wetu wanaojiandaa kuwakabili Nigeria kesho jumapili kwenye uwanja wa Taifa jijini
Dar es salaam majira ya saa 10:00 jioni.
Ngongoro
wamefikia raundi ya pili baada ya kuwatoa Kenya kwa penati 4-3 kufuatia kutoka
suluhu ya bila kufungana katika mechi
zote mbili.
Kocha
wa Ngorongoro, John Simkoko anakabiliana na Fly Eagles wenye historia nzuri
katika soka la vijana barani Afrika.
Hii
itakuwa mechi muhimu kwa Tanzania, hivyo jambo jema kwa mashabiki ni kujitokeza
kuwashangilia vijana hao kama walivyoomba.
Mechi
dhidi ya Kenya haikuwa na watu wengi sana, lakini mechi dhidi ya Nigeria
mashabiki wana nafasi kubwa ya kuwapa motisha wachezaji kwa kujitokeza kwa
wingi uwanjani kwasababu wana nafas kubwa ya kuisaidia timu.
Mashabiki
ni mchezaji wa 12, TFF wamefanya kazi yao, John Simkoko kafanya kazi yake,
wachezaji wamejiandaa kwa nafasi zao na wataingia kushindana kesho, watu pekee
waliosalia kutimiza wajibu wao ni mashabiki wa soka.
Watanzia
twendeni tukaishangilie timu yetu kwasababu ikipata mafanikio itakuwa faida na
heshima kwa Tanzania.
Kutokana
na ubora wa Nigeria, kuna ulazima mkubwa wa Ngongoro kupata magoli angalau
matatu nyumbani ili kujiweka mazingira mazuri ya kufuzu katika mechi ya
marudiano.
Vijana
wetu watambue kuwa kuna utofauti mkubwa wa Nigeria na Kenya, hivyo watatakiwa
kuwa na nidhamu kubwa uwanjani.
Kwa
vile Simkoko yupo nyumbani, bila shaka atataka kumilikia mpira na kushambulia zaidi ili
kupata magoli mengi, lakini wakati vijana wake wakicheza hivyo, ni lazima
kuzingatia ubora wa Nigeria kwasababu wanaweza kubadili matokeo wakati wowote.
Hakuna
haja ya kuwaogopa Nigeria, kikubwa wachezaji wetu wajiamini na kuona wao ni
bora zaidi.
Walinde
lango lao, wacheze mpira na kushambulia. Kama watafanya kazi hizi tatu
tunatarajia kupata matokeo. Lakini cha msingi zaidi kila nafasi watakayoipata
waitendee haki.
Nidhamu
ya mpira itahitaji sana kwasababu Nigeria ni watu makini na wanajua kutumia
makosa ya wapinzani, na hii si tu kwa timu za vijana, hata timu ya wakubwa
wanaweza kucheza sana mpira.
Fainali
hizo za 19 za Afrika zitafanyika mwakani nchini Senegal zikishirikisha timu
saba zitakazofuzu kwenye mechi za mchujo, na Senegal wanaoingia moja kwa moja
kutokana na kuwa wenyeji.
Viingilio
katika mechi hiyo ni sh. 2,000 kwa sehemu zote wakati upande wa VIP itakuwa sh.
5,000. Tiketi zitauzwa uwanjani siku ya mechi katika magari maalumu.
0 comments:
Post a Comment