Na
Baraka Mpenja, Dar es salaam
BEKI na nahodha wa zamani wa Yanga sc, Ally Mayay
Tembele ameshauri viongozi wa timu za Tanzania kuachana na mfumo wa kutoa mikataba
mifupi kwa makocha wao kwasababu zipo katika harakati za kutafuta maendeleo.
Mayay
ameueleza mtandao huu kuwa kwa bahati mbaya klabu zetu hazina utamaduni na
falsafa zao za kucheza mpira, hivyo kila mwalimu anakuja na mfumo wake.
Akitumia
mfano wa Simba sc, Mayay alisema ndani ya kipindi kifupi wamekuwa na makocha wanne
na kupata athari kubwa katika michuano ya ligi kuu.
“Kumbuka
kwa mfululizo, Simba wamebadili makocha. Aliondoka Milovan Circovic, akaja
Patric Liewig, baadaye wakamleta Abdallah Kibadeni, na mwanzoni mwa mzunguko wa
pili wa msimu uliopita akaletwa Dravko Lofarusic”.
“Kwa
asimilia kubwa kufanya vibaya kwa Simba kumechangiwa na athari kubwa ya
mabadiliko ya makocha”.
“Kila
kocha ana falsafa yake. Na kwa bahati nzuri Simba wana wachezaji wengi vijana ambao
ni rahisi kumeza falsafa za makocha makocha wao”.
“Vijana
kama Ramadhan Singano, Ndemla, Mkude, Chanongo wanafundishika kirahisi kutokana
na umri wao”.
“Milovan
ana falsafa yake ambayo huitumia. Kuna aina ya mpira anataka wachezaji wake
wacheze, na wachezaji wanaanza kuzoea mfumo huo”.
“Ghafla
analetwa mfaransa Liewig, naye anaanza upya na mfumo wake, wachezaji wanaanza
kuuzoea, mara analetwa Kibadeni mwenye mfumo wake”.
“Wachezaji
wakiwa katika harakati za kuuzoea mfumo wa kibadeni, ghafla analetwa Mcroatia
Loga. Naye analeta mfumo wake”.
“Haya
yanatokea kwasababu klabu haina falsafa yake. Huwezi kujua upi ni utamaduni wa
uchezaji wa Yanga ua Simba”.
“Timu
zinabadilika badilika kutokana na aina ya walimu wanaoletwa”. Alifafanua Mayay.
Aidha,
aliongeza kuwa kwa wenzetu kila klabu ina falsafa yake, huku akitolea mfano wa
soka la Barcelona.
Mayay alisema hata aje mwalimu kutoka wapi, ni
ngumu kubadili mfumo wa soka la Barcelona na kinachotakiwa kwa makocha ni kuingiza baadhi ya mbinu za
kiufundi lakini si kubadili mfumo mzima wa uchezaji.
“Angalia
Guardiola anavyohangaika kuibadili Bayern yenye utamaduni wake. Inakuwa ngumu
kwasababu wamejengwa katika falsafa fulani na utamaduni wa soka la Ujerumani”.
Akizungumzia
kuondoka kwa kocha wa Yanga baada ya kuiongoza klabu kwa miezi mitano tu, Mayay
alisema si jambo geni kwasababu amemaliza mkataba wake, lakini akasema litaleta
athari kwa klabu.
“Yanga
wamekaa na kocha wao miezi mitanotu baada ya kumaliza mkataba wake wa miezi sita.
Pluijm alianza kuijenga Yanga katika misingi fulani”.
“Ilikuwa
inacheza mpira tofauti na ilivyokuwa kwa Ernie Brandts, sasa wakati wachezaji
wakiiva katika mfumo wa Pluijm wanajikuta wakianza upya na kocha mpya msimu ujao”.
“Kama
atakuja na mfumo mpya, maana yake Yanga wataanza upya kiuchezaji”.
“Nawashauri
wawe na tabia ya kuwapa makocha mikataba mirefu, angalau kuanzia miaka miwili.”
Mei 8 mwaka huu, kocha mkuu wa Young
Africans, Mholanzi, Hans Van der Pluijm aliondoka Yanga baada ya kupata kazi
mpya nchini Saudi Arabia na tayari alishaaga na kuondoka zake.
Pluijm aliyejiunga na Yanga mapema januari mwaka
huu umepata shavu hilo katika klabu ya Al Shoalah FC inayoshiriki ligi kuu soka
nchini Saudi Arabia.
Yanga chini ya Pluijm ilimaliza katika nafasi ya
pili, huku Azam fc chini ya kocha Mcameroon, Joseph Marius Omog wakibeba taji
lao la kwanza tangu wapande ligi kuu msimu wa 2008/2009.
0 comments:
Post a Comment