KLABU ya Manchester City imebeba taji la ligi kuu nchini England kwa mara ya pili katika misimu mitatu na mchana wa leo watafanya sherehe kubwa katika dimba lao la Etihad kushangilia mafanikio hayo.
Magoli ya Samir Nasri na Vincent Kompany yaliisaidia Man City kushinda mabao 2-0 dhidi ya West Ham na kufanya ushindi wa mabao 2-1 waliopata Liverpool kwenye uwanja wa Anfield dhidi ya Newcastle usiwe na maana yoyote.
Baada ya kipyenga cha mwisho kupulizwa, maelfu ya mashabiki wa Man City waliingia uwanjani kuwapongeza mashujaa wao.
Tazama picha hapo chini jinsi Man City walivyoshangilia kubeba ubingwa wa EPL.
Mabingwa wa England: Manchester City wamebeba ndoo ya pili katika misimu mitatu baada ya kuifunga West Ham mabao 2-0
Nahodha wa ajabu: Vincent Kompany akibeba kombe la ligi kuu
Sherehe: Vincent Kompany akibeba kombe la ligi kuu kuashiria mwisho wa msimu wa mafanikio kwa Man City
Washikaji: Joleon Lescott, Vincent Kompany na Joe Hart wakipiga picha pamoja kwenye chumba cha kubadilishia nguo
Mwalimu na kamanda: Nahodha Vincent Kompany na bosi wake Manuel Pellegrini wakishika kombe la ligi kuu
Sergio Aguero akinyanyua kombe kwa mara ya pili akiwa na Man City
Mzee juu juu: Wachezaji wa Man City wakimbeba na kumrusha hewani Manuel Pellegrini
Furaha: Hata Manuel Pellegrini alitabasamu alipobebwa na wachezaji wake
Wakati wa furaha: Pellegrini akipozi katika picha na kombe lake la kwanza Man City
Maneno ya shukurani
Maelfu ya mashabiki wa Man City walivamia uwanja wa Etihad baada ya kipyenga cha mwisho
Mzee wa familia: Kompany akiwa katika pozi la picha kwa kushika kombe la ligi kuu pamoja na familia yake
Shangwe tupu Etihad, ubingwa raha sana
0 comments:
Post a Comment