Wednesday, May 14, 2014



DSC05597
Na Baraka Mbolembole
Golikipa wa Shaaban Kado tayari ameanza mazoezi baada ya kuondoa plasta ngumu ( P.O.P) ambayo alifungwa tangu mwezi machi baada ya kuvunjika sehemu ya mkono wake.
Akizungumza na mtandao huu kipa  huyo aliyemaliza mkataba wake na timuya Coastal Union yaTanga, amesema tayari ameanza kujifua wakati akitafakari wapi pa kwenda kucheza msimu ujao.
Amekanusha kila uvumi unaomuhusisha yeye na klabu za Azam FC na Simba SC, huku akisema kuwa ana malengo tayari hivyo ukifika wakati atafikia maamuzi.
“ Kwasasa naendelea vizuri, nimeanza mazoezi binafsi.” Anasema mlinda mlango huyo wa Tanzania ambaye aliwahi kushinda tuzo ya kipa bora wa ligi kuu katika msimu wa mwaka 2008/09 akiwa na kikosi cha Mtibwa Sugar. Kado yupo huru tangu April 24, lakini bado hajawa tayari kuweka wazi ni wapi atacheza kuanzia msimu ujao.
“ Mimi sijasikia chochote kuhusu kutakiwa na timu hizo ( Simba , Azam) hivyo siwezi kuzungumza lolote. Nina malengo yangu hivyo wakati ukifika kila kitu kitakuwa wazi” anasema, Kado ambaye ameitwa mara kadhaa katika timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars na hadi anaumia alikuwa katika kikosi hicho ambacho kilicheza na timu ya Nambia, mapema mwezi machi mwaka huu.
Stars itacheza na Zimbabwe siku ya jumapili hii katika uwanja wa  Taifa, Dar es Salaam katika mchezo wa kwanza kati ya miwili ya mtoano kuwania kufuzu kwa hatua ya makundi ya kufuzu kwa fainali za Mataifa ya Afrika, 2015, Nchini, Morocco, Kado kwa upande wake anasema ni wakati wa kuisapoti timu hiyo na ana imani kuwa kila mchezaji tayari anajua majukumu yake kuelekea katika mchezo huo.
“ Ni, wajibu kuiombea timu yetu ipate matokeo mazuri katika uwanja wa nyumbani. Kila mchezaji atakuwa anafahamu majukumu yake na kwanini yupo pale ( Stars). Muhimu ni kupata ushindi wa kutosha. Brazil iliyotajwa na Scorali inaweza kutwaa ubingwa bila kuwa na wachezaji wazoefu “
Wakati michuano ya kombe la dunia ikitaraji kuanza kutimua vumbi lake, Juni, mwaka huu katika nchi ya Brazil, Kado kama ilivyo kwa Watanzania wengi naye tayari ana timu ambayo ataisapoti katika michuano hiyo ya 21.
“ Mimi ni shabiki wa Brazil, timu imara na ni timu ya michuano. Naipenda tu, Brazil namna wanavyocheza na vipaji walivyonavyo. Sina shaka na uteuzi wa kocha Scorali ( Luiz) katika uteuzi wake, naamini amefanya machaguo sahihi ya wachezaji, na tusisahau kuwa Brazil ndiyo ‘ wafalme wa kandanda duniani’, ni timu yenye vipaji vingi hivyo unapoona kocha anawaacha wachezaji kama, Ricardo Kaka’ na Robinho basi jua tayari amekuwa na mbadala wao”

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video