Friday, May 2, 2014



 Saha backs Giggs for full-time Manchester United job
MSHAMBULIAJI wa zamani wa Manchester United, Luis Saha ameunga mkono Ryan Giggs kupewa nafasi ya kuwa kocha wa kudumu Old Trafford.

Giggs aliteuliwa kuwa kocha wa muda wa Man United baada ya David Moyes kutimuliwa mwezi uliopita akiwa amefanya kazi miezi 10 tu katika mkataba wake wa miaka 6.

Mechi ya kwanza ya United chini ya mkongwe huyo raia wa Welsh ilishinda mabao 4-0 dhidi ya Nowrich City kwenye dimba la Old Trafford jumamosi iliyopita na atakuwa kwenye kibarua chake kwa mechi tatu zilizosalia.

Kocha Mholanzi, Louis van Gaal amekubali kazi ya kuifundisha Man United, huku Giggs akitarajiwa kuwa sehemu ya benchi lake la ufundi, lakini Saha ametaka mchezaji mwenzake huyo wa zamani kupewa nafasi hiyo.

“Namjua Ryan atakosa nafasi na nadhani anastahili kupewa ukocha wa kudumu”. Saha ameuambia mtandao wa Sky Sports News.

“Ni fursa kubwa kwake. Kiukweli ana sifa zote, ana mvuto na ni mstahimilivu. Hakuna wasiwasi juu ya hilo”.

“Amekosa uzoefu tu, lakini unapocheza Manchester United kwa zaidi ya miaka 20 unajua namna ya kufanya kazi”.

“Labda siko sahihi, lakini nadhani inahuzunisha, nadhani angepewa mwezi mwingine kutulia na kuonesha kuwa ni chaguo sahihi. Mechi nne hazitoshi”.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video