Aishi Manula |
Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
KOCHA wa timu ya Taifa ya vijana chini ya miaka 20, Ngorongoro Heroes, John Simkoko amesema kikosi chake kipo tayari kukabiliana na Nigeria hapo kesho katika Mechi ya kwanza ya raundi ya pili ya michuano ya Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 20.
Simkoko amesema michezo miwili iliyopita dhidi ya
Kenya, kikosi chake kilikuwa na matatizo katika safu ya ushambuliaji, lakini
kwa sasa amenoa safu yake na kuiongezea makali zaidi.
“Tumejiandaa vizuri na kufanya marekebisho ya safu
ya ushambuliaji. Tunafahamu kuwa Nigeria ni timu nzuri na kila mtu anajua,
lakini tutaingia kushindana na matokeo yatakayotokea tutayaheshimu”. Alisema
Simkoko.
Kwa upande wake nahodha wa kikosi hicho, Aishi
Manula amewaomba mashabiki wa soka kujitokeza kwa wingi kuwashangilia na
kuepuka kuwazomea pale wanapofanya makosa.
“Kuna wachezaji wengi hawana uzoefu na hawajazoea
presha ya kuzomewa. Tukianza mechi halafu wakakosea na kozemewa watapoteza
morali”.
“Imefikia wakati wa kuiunga mkono timu na kuacha
kuwazomea wachezaji. Tumejiandaaa vizuri na tuko tayari kwa mechi”. Alisema
Manula.
Viingilio katika mechi hiyo ni sh. 2,000 kwa
sehemu zote wakati upande wa VIP itakuwa sh. 5,000. Tiketi zitauzwa uwanjani
siku ya mechi katika magari maalumu.
Afisa habari wa shirikisho la soka Tanzania, TFF,
Boniface Wambura alisema lengo la kuweka kiingilio kidogo ni kuwapa nafasi
mashabiki wote kuiona timu yao.
“Kiingilio hakijawekwa kwa ajili ya gharama za
mechi. Gharama ni kubwa zaidi, lakini tumeweka kiingilio kidogp ili kutoa
nafasi kwa mashabiki wote”.
“Wito wetu kwa mashabiki ni kuwaomba wafike kesho
kwa wingi ili kuwapa motisha wachezaji”. Alisema Wambura.
Fainali hizo za 19 za Afrika zitafanyika mwakani
nchini Senegal zikishirikisha timu saba zitakazofuzu kwenye mechi za mchujo, na
Senegal wanaoingia moja kwa moja kutokana na kuwa wenyeji.
0 comments:
Post a Comment