KWA
mwaka wa pili mfululizo, mwanasoka bora wa dunia Cristiano Ronaldo ametajwa
kushindania tuzo ya `kiatu cha dhahabu` ambapo atapambana na Andres
Iniesta, Franck
Ribery, Andrea
Pirlo na Yaya
Toure.
Tuoz
hiyo ya kimataifa hutolewa mara moja kwa
mwaka na inatolewa kwa wachezaji wenye umri zaidi ya miaka 28 ambao wamekuwa
katika mafanikio binafsi mfululizo na
mafanikio ya klabu zao, huku utu wao pia ukihusika.
Mbali
na nyota huyo wa Real Madrid, orodha ya wachezaji iliyoandaliwa ni: Thierry
Henry, Iniesta, Manuel Neuer, Pirlo, Ribery, Wayne Rooney, Toure, Thiago Silva
na mwanasoka wa kike kutoka Brazil Marta.
Kura
zitaanza kupigwa agosti 24 mwaka huu, huku sherehe za kutoa tuzo hiyo
zikifanyika jumapili ya Oktoba 13 mjini Monaco.
Mshindi atachaguliwa na mashabiki kupitia
Tovuti ya Golden Foot au ukurasa wa facebook wa Golden Foot.
Tuzo
hii ilianzishwa mwaka 2003 na mshindi wa mwaka huu ataungana na wachezaji wengine
waliowahi kutwaa ambao ni Roberto Baggio, Pavel Nedved, Andriy Shevchenko,
Ronaldo, Alessandro Del Piero, Roberto Carlos, Ronaldinho, Francesco Totti,
Ryan Giggs, Zlatan Ibrahimovic na Didier Drogba.
0 comments:
Post a Comment