CRISTIANO
Ronaldo anaamini kuwa nyota wa Barcelona, Mbrazil, Neymar atakuwa mchezaji bora
wa dunia.
Wakatalunya
walimsajili kinda huyo mwenye miaka 22 kutoka klabu ya Santos ya Brazil kwa dau
linalokadiriwa kuwa paundi million 87.2 na amefunga mabao 9 katika mechi za
ligi na kutoa pasi za mwisho 8 katika mechi zake 25 alizocheza.
Licha
ya Rea Madrid kuwa wapinzani wakubwa kutafuta ubingwa wa La Liga kuliko
Barcelona, Ronaldo anadhani kuwa nyota huyo wa Brazil atakuwa moja ya wachezaji
nyota zaidi duniani.
“Namtazama
Neymara kama mchezaji mkubwa,” aliwaambia SportsTVnews.
“ Nadhani kwa kipindi cha sasa ameonesha kuwa atakuwa mchezaji mkubwa kwa
baadaye”.
“Alichelewa
kufiti katika mfumo wa Barcelona kiuchezaji, alikuwa na matatizo mwanzoni,
lakini sina wasiwasi juu ya yeye kuwa
mchezaji bora wa dunia au bora zaidi na zaidi”.
Ronaldo
mwenye miaka ya 29 alipoulizwa hatima ya timu ya taifa ya Ureno kwenye fainali
za kombe la dunia mwaka huu nchini Brazil alikiri kuwa nchi yake imepangwa
kundi ngumu zaidi na timu za Ujerumani, Ghana na Marekani.
“Sisi
hatupewi nafasi kubwa,” alisema. “Lakini tutajitahidi kulifurahia. Tunajua tupo
kundi gumu, kwa maoni yangu ni kundi lenye mataifa makubwa zaidi duniani”.
“Tunatakiwa
kwenda hatua kwa hatua. Tutakuwa na mchezo mgumu wa kwanza dhidi ya Ujerumani,
halafu tutacheza na Ghana na kumalizia na Marekani. Baada ya hapo tutaona”.
0 comments:
Post a Comment