Monday, May 5, 2014


Bonge la bao: Nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo amefunga bonge la bao jana katika sare ya 2-2 na Valencia

MCHEZAJI bora wa dunia, Mreno, Cristiano Dos Santos Aveiro Ronaldo jana alifunga bao la hatari sana na kuinusuru Real Madrid kupoteza mechi nyumbani.
Valencia ilionekana kubeba pointi zote tatu Uwanja wa Santiago Bernabeu, lakini mshindi huyo wa Ballon d'Or aliinusuru timu yake tena, alipounganisha krosi ya Angel di Maria kwa utaalamu wa hali ya juu. 
Mathieu alianza kuifungia Valencia dakika ya 44, lakini Sergio Ramos akaisawazishia Real Madrid dakika ya 59na Parejo akawafungia wageni bao la pili, kabla ya Ronaldo kufunga lake la 50 msimu huu. 
Licha ya Atletico kufungwa 2-0 na Levante jana, bado ipo kileleni mwa La Liga kwa pointi zake 88 za mechi 36, ikifuatiwa na Barcelona pointi 85 mechi 36 wakati Real sasa ni ya tatu kwa pointi zake 83 za mechi 35.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video