
KOCHA
wa Liverpool, Brendan Rodgers bado ana matumaini ya kuchukua ubingwa licha ya
kutolewa kileleni na Manchester City.
Vijana
wa Manuel Pellegrini walipanda kileleni kwa wastani mzuri wa mabao ya kufunga
na kufungwa baada ya kushinda mabao 3-2 dhidi ya Everton kwenye uwanja wa
Goodison Park jumamosi iliyopita, huku wakisubiri mechi ya leo baina ya
Liverpool na Crystal Palace.
Kama
timu zote zitashinda mechi zao mbili za mwisho, bingwa atapatikana kwa tofauti
ya magoli, na Rodgers anaamini timu yake itafunga mabao mengi zaidi katika
mechi zake za mwisho ili kujiweka mazingira mazuri ya kubeba taji.
“Kama
kuna timu itakayofunga mabao mengi na kubadili mambo tutakuwa sisi”. Aliwaambia
waandishi wa habari.
“Hakuna
swali hapo. Hilo ndio lengo letu. Hakuna swali kuhusu hilo. Nimeona siku za
nyuma. Chelsea waliwafunga Wigan 8-0 katika mchezo wa mwisho wa msimu (kipindi
Chelsea walipotwaa ubingwa mwaka 2010).
“Siwadharau
hata kidogo Newcastle, lakini kama kuna timu yoyote iliyoonesha uwezo wa
kufunga magoli, ni sisi. Sisi sio watu wa 1-0. Tulionesha hilo mwanzoni mwa
msimu, lakini tulichokionesha tangu mwanzoni ni kwamba tunao uwezo wa kufunga
magoli mengi”. Aliongeza Rodgers.
City
wanajiombea ushindi katika mechi zao mbili za mwisho dhidi ya Aston Villa na
West Ham, zote zitapigwa Etihad, lakini Rodgers anaamini hawatazoa pointi zote
sita.
“Ni
kazi ngumu kwa City,” Aliongeza. “Aston Villa ni timu bora, tena inayoshambulia kwa kushitukiza na wanakuwa
wazuri zaidi wanapokuwa ugenini, na West Ham siku hiyo watatoa upinzani
mkubwa”.
Rodgers
pia alisisitiza kuwa kikosi chake hakijaathirika hata kidogo na matokeo ya kupigwa
mabao 2-0 na Chelsea wiki iliyopita kwenye uwanja wa Anfield.
“Hakuna
aliyekata tamaa na matokeo ya wiki iliyopita; si wachezaji, viongozi wala
mashabiki”. Alieleza.
“Baada
ya mchezo kuna siku nyingi za kujipanga kwasababu mabingwa siku zote wanachukua
baiskeli yao na kuanza tena safari na hiki ndicho kitu nilichopandikiza katika
timu hii”
0 comments:
Post a Comment