Saturday, May 17, 2014


Bado gonjwa; Cristiano Ronaldo ameendelea kuwa nje kwa maumivu ya nyama   

  REAL Madrid imemaliza kwa heshima msimu wa La Liga baada ya kuifunga mabao 3-1 Espanyol Uwanja wa Santiago Bernabeu jioni hii.
Ushindi huo unaifanya Real imalize msimu huu wa La Liga na pointi 87 baada ya kucheza mechi zote 38 na inaweza ikawa ya pili ya tatu baada ya mechi zote, itategemea na matokeo ya mchezo kati ya Barcelona na Atletico Madrid unaoendelea hivi sasa Uwanja wa Camp Nou.
Mabao ya Real yalifungwa na Gareth Bale dakika ya 64 akimalizia pasi ya Karim Benzema, Alvaro Morata mawili dakika ya 86 na 90, wakati bao pekee la Espanyol lilifungwa na Pizzi dakika ya 90 pia.
Real ilendelea kumkosa mwanasoka bora wa dunia, Cristiano Ronaldo anayesumbuliwa na maumivu ya nyama, ambaye awali iliripotiwa angecheza sehemu ya mchezo wa leo.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video