Balaa hilo!: mchezaji wa Valladolid, Humberto Osorio akifunga bao la kusawazisha dakika za lala salama dhidi ya Real Madrid.
BAO
la kusawazisha la Humberto Osorio katika dakika za mwisho limepunguza
matumaini ya Real Madrid kutwaa ubingwa wa La Liga msimu huu.
Real
walitegemea kuongeza presha kwa vinara Atletico Madrid, lakini sare ya
1-1 dhidi ya Valladolid usiku huu imewafanya waendelee kukaa nafasi ya
tatu pointi 4 nyuma ya mahasimu wao wa jiji na pointi moja nyuma ya
Barcelona waliopo nafasi ya pili katika msimamo wa La Liga.
Timu zote zimebakiwa na mechi mbili na kama Real Madrid wangeshinda leo wangekuwa katika mazingira mazuri ya kutwaa ubingwa.
Matokeo ya leo yamefungua milango kwa Barcelona, na sasa wanajua kuwa wanaweza kutwaa ubingwa kama wataifunga Atletico Madrid mechi ya mwisho, huku wakitakiwa kushinda dhidi ya Elche siku ya jumapili ugenini.
Hali tete: Matumaini ya Real Madrid kutwaa ubingwa yamepungua baada ya kushindwa kuwafunga Valladolid.
Mechi ilianza vibaya kwa Real Madrid baada ya nyota wake na mwanasoka bora wa dunia Cristiano Ronaldo kupata maumivu ya nyama za paja na kutolewa nje.
Madrid walianza kuongoza baada ya Sergio Ramos kufunga bao kwa mpira wa adhabu ndogo.
Bao hili lilikuwa muhimu sana kwa Ramos ambaye anasherekea kuzaliwa kwa mwanaye hapo jana jumanne na mechi yake ya 400 akiwa na Real Madrid.
Beki wa Real Madrid, Sergio Ramos akishangilia baada ya kufunga bao la kuongoza dhidi ya Real Valladolid
Beki wa Real Madrid Sergio Ramos akifanya yake
Ramos akishangilia bao lake na kocha wa Real Madrid Carlo Ancelotti
MSIMAMO WA LA LIGA KWA TIMU 10 ZA JUU HUU HAPA
Spanish La Liga | LOGS
Pos | Team | P | W | D | L | GF | GA | GD | Pts |
1 | Atlético de Madrid | 36 | 28 | 4 | 4 | 75 | 24 | 51 | 88 |
2 | Barcelona | 36 | 27 | 4 | 5 | 99 | 32 | 67 | 85 |
3 | Real Madrid | 36 | 26 | 6 | 4 | 101 | 35 | 66 | 84 |
4 | Athletic Club | 36 | 20 | 8 | 8 | 65 | 38 | 27 | 68 |
5 | Sevilla | 36 | 17 | 9 | 10 | 66 | 50 | 16 | 60 |
6 | Real Sociedad | 36 | 16 | 10 | 10 | 60 | 52 | 8 | 58 |
7 | Villarreal | 36 | 15 | 8 | 13 | 54 | 43 | 11 | 53 |
8 | Valencia CF | 36 | 12 | 10 | 14 | 49 | 50 | -1 | 46 |
9 | Celta de Vigo | 36 | 13 | 7 | 16 | 46 | 52 | -6 | 46 |
10 | Levante | 36 | 11 | 12 | 13 | 33 | 42 | -9 | 45 |
0 comments:
Post a Comment