RAIS wa FIFA, Sepp Blatter amekiri kuwa walifanya
makosa kuwapa Qatar uenyeji wa fainali za kombe la dunia za mwaka 2022.
Qatar waliwashinda wapinzani wao Marekani, Korea kusini,
Japan na Australia, lakini maamuzi ya FIFA kuwapa nafasi ya kuhodhi michuano
hiyo yalikoselewa vikali tangu yalipothibitishwa desemba mwaka 2010.
Sababu kubwa ya watu wengi kupinga Qatar kuwa
mwenyeji wa kombe la dunia ni kwasababu ya joto kali majira ya kiangazi ambapo
kombe hilo hufanyika.
Hata hivyo FIFA walipotangaza maamuzi yao, mwaka
mmoja baada iliibuka kashfa ya rushwa ambapo ilielezwa kuwa Qatar waliwahonga
maofisa wa FIFA na kuwepa uenyeji wa fainali hizo za mwaka 2022.
Aidha, shiriki la kutetea haki za binadamu la
kimataifa limewataka FIFA kuingilia kati kwani kuna taarifa za kunyanyaswa kwa
wafanyakazi wanaojenga viwanja katika taifa hilo la Gulf.
Siku za nyuma, Blatter alikuwa anatetea uamuzi wa
FIFA kuwa ulikuwa sahihi kuwapa uenyeji Qatar, lakini kwasasa amekiri kuwa ilikuwa
makosa.
“Kiukweli yalikuwa makosa (kuwapa uenyeji wa kombe
la Dunia Qatar)”. Blatter amewaambia RTS.
“Lakini wote tunajua kuwa makosa yanatokea katika
maisha”.
“Ripoti za idara ya ufundi kutoka Qatar zilieleza
kuwa majira ya kiangazi kuna joto kali sana. Hata hivyo haikuzuia kamati kuwapa
uenyeji wa fainali za kombe la dunia, tena kwa kura nyingi”.
0 comments:
Post a Comment