
Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
KOCHA wa Tanzania Prisons, `Wajelajela`, Mkongwe
David Mwamwaja amekabidhi ripoti yake kwa viongozi ili kuanza mipango ya
usajili mapema.
Katibu mkuu wa klabu hiyo, Inspekta Sadick Jumbe
amesema Mwamwaja amekabidhi ripoti yenye mapendekezo yake siku mbili zilizopita
na tayari ameshaiwasilisha makao makuu kwa lengo kuipitisha na kuanza
utekelezaji.
Jumbe alibainisha kuwa Mwamwaja amependekeza
kuongezewa nguvu katika sehemu tatu ambazo ni nafasi ya mlinda mlango, ulinzi
na ushambuliaji.
“Mwalimu ameshauri tutafute kipa mwenye uzoefu na
kiwango cha juu”.
“Pia tuongeze beki wa kati ili kuimarisha safu ya
ulinzi. Zaidi imetuomba kuongeza nguvu
kwenye safu ya ushambuliaji ”.
“Angalia timu ilikuwa inamtegemea zaidi Michael
Peter katika ufungaji, sasa Mwamwaja amesema lazima atafutwe mtu mwingine wa
kusaidiana na kijana huyu”. Alisema Jumbe.
Jumbe aliongeza kuwa utaratibu wao ni kuwa, kila wanapopokea ripoti ya mwalimu huwa
wanaipeleka makao makuu ya Jeshi la Magereza ambao huijadili na kuipitisha.
Wakishaipitisha wanairudisha kwa viongozi wa klabu
tayari kwa utekelezaji.
“Siku mbili tatu zijazo natarajia kurudishiwa
ripoti hii, tunaanza usajili mapema”. Alisema Jumbe.
Akizungumzia maaandalizi ya msimu ujao, Jumbe
alisema wanajipanga mapema ili kufuta makosa ya nyuma.
“Misimu miwili tumekuwa tukipambana nafasi za
chini na pengine kukwepa kushuka daraja”.
“Tumeshamwambia Kocha wetu Mwamwaja kuwa msimu
ujao tunahitaji kushika nafasi za juu”.
“Ili kufanikiwa hili, tunatarajia kutekeleza kila
pendekezo lake kwa asilimia mia 100”. Aliongeza Jumbe.
Hata hivyo, hakusita kuwashukuru mashabiki wao kwa
sapoti kubwa waliyoipatia klabu yao hadi kufanikiwa kubakia ligi kuu.
“Natumia fursa hii kuwapongeza kwa moyo wa
uvumilivu. Tunajua wanaipenda timu yao, kikubwa, tunajipanga vizuri msimu ujao
na tunawategemea sana”. Alimaliza Inspekta Jumbe.
0 comments:
Post a Comment