Sunday, May 4, 2014



http://www.fullshangweblog.com/wp-content/uploads/2014/04/IMG_0293.jpg
Na Baraka Mpenja, Dar es Salaam
MAAFANDE wa Polisi Morogoro wanahitaji kusajili wachezaji vijana ili kuendana na kasi ya ligi kuu soka Tanzania bara msimu ujao.
Afisa habari wa klabu hiyo, Clemence Banzo amesema ligi kuu ni ngumu kutokana na timu kuwa imara kama vile Mbeya City fc, Azam fc, Yanga, Simba na nyingine, hivyo lazima wafanye usajili wa wachezaji wa kuwasaidia.
Banzo alisema wanataka kusajili wachezaji vijana kwasababu wana uchu wa mafanikio na malengo yao ni kutafuta majina katika ulimwengu wa soka.
“Kwa siku za nyuma tulikuwa tunachukua wakongwe waliochoka kutoka Simba na Yanga na klabu nyingine, kumbe wameshafikia kikomo katika mpira”
“Wanapofika kwenye timu wanaonekana kuwa na maana, lakini hakuna mchango wowote wanaotoa kwasababu mpira wao umekwisha”.
“Safari hii tunakuja upya, tunasajili damu changa ili kupambana na timu kama Mbeya City”. Alisema Banzo.
Hata hivyo alipoulizwa kama watakuwa tayari kuvumilia kwa aina ya wachezaji vijana, Banzo alisema kwa bahati nzuri timu yao inaposhuka daraja haikuwa mbaya na  wataongezea nguvu tu.
“Waliondoka wachezaji wachache, wengi wana uzoefu na ligi kuu. Tutaongeza vijana wachache ili kukiongezea makali kikosi chetu”.
Banzo aliwashukuru mashabiki wa soka mkoani Morogoro kwa kuwa msaada mkubwa kwa timu na kuwahakikishia kuwa uongozi unajipanga kuiweka timu ligi kuu kwa muda mrefu.
“Baada ya kushuka Reli ya Morogoro ikabaki Polisi, angalia Mtibwa wapo Manungu kule. Mashabiki wamekosa ligi hapa mjini, na wamejifunza nini maana ya ushabiki kutoka kwa Mbeya City fc”.
“Kwasasa kwenye vikao vingi utakuta raia ndio wanaotoa maoni mengi, kwa kutambua hilo, tunawaahidi kuijenga timu vizuri na tunapokosea wasiache kutukosoa”.
Polisi Morogoro ni moja ya timu tatu zilizopanda ligi kuu soka Tanzania bara kwa msimu wa 2014/2015, huku nyingine zikiwa ni Ndanda fc kutoka mkoani Mtwara na Stand United ya Shinyanga.
Timu tatu zilizoshuka msimu uliopita na kuzipisha timu mpya ni wauza mitumba wa Ilala, Ashanti United, Maafande wa JKT Oljoro na Rhino Rangers.
Msimu ujao mashabiki wa Arusha na Tabora watakuwa wanaisikia ligi kuu kwenye redio na kuiona kwenye televisheni.
Lakini kwa Dar es salaam licha ya kushuka kwa Ashanti, burudani ipo pale pale kwasababu ya wanaume Yanga, Simba na Azam fc.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video