PEP Guardiola anapigana vita ya ndani kwa ndani katika klabu yake ya Bayern Munich baada ya kazi yake kuingia dosari msimu huu katika michuano ya UEFA, huku akihusishwa kuelekea ligi kuu soka nchini England.
Mhispani huyo alifika ujerumani mwanzoni mwa msimu huu na tayari ameshashinda taji la Bundesliga, UEFA Super Cup na kombe la FIFA la klabu bingwa ya Dunia.
Lakini kocha huyo wa zamani wa Barcelona anapigana vita ya kukishawishi kikosi chake kiendeleza mafanikio waliyoyapa siku za karibuni.
Presha juu: Pep Guardiola yupo hatarini kupoteza umoja katika vyumba vya kubadilishia nguo katika klabu ya Bayern Munich
Licha ya kushinda makombe matatu msimu huu, kipigo cha aibu walichokipata Bayern kutoka kwa Real Madrid hatua ya nusu fainali ya UEFA kimeibua maswali juu ya hatima yake ya baadaye.
Kuna mitazamo kuwa timu imeshuka kiwango chini ya Guardiola, na hii inahusishwa na kipigo kutoka kwa Carlo Ancelotti.
Mbaya sana kuna kundi la wachezaji wanaanza kuunga mkono mitazamo hii , hivyo Guardiola kuwa hatarini kupoteza umoja wa wanandinga wake.
Kuna hisia miongoni mwa watu kuwa umoja mkubwa wa timu ilioachwa na Louis van Gaal na Jupp Heynckes umeanza kupotea chini ya Guardiola.
Gwiji wa soka wa Bayern Franz Beckenbauer wiki iliyopita alionesha kuumizwa sana na kiwango cha timu hiyo kufuatia kipigo walichoambulia kutoka kwa Real.
0 comments:
Post a Comment