Dzeko akiungana na wachezaji wa Man City kushangilia bao lake la pili jana usiku
Vitu vya hatari vya nahodha wa Man City Kompany
Hataki kutazama: Manuel Pellegrini yupo katika asilimia kubwa ya kutwaa taji la ligi kuu.
KOCHA
wa Manchester City, Manuel Pellegrini amewasifu wachezaji wake kwa kuwa wavumilivu
katika ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Aston Villa na kuukaribia ubingwa wa ligi
kuu nchini Engalnd msimu.
Mabao
ya kipindi cha pili yaliwahakikishia Man City ushindi na kurejea kileleni kwa
pointi mbili mbele dhidi ya majogoo wa jiji, Liverpool, huku wakisaliwa na mecho moja ya mwisho dhidi
ya West Ham siku ya jumapili.
Vijana
wa pellegrini walichanganyikiwa baada ya kuoneshwa upinzani mkubwa na Villa
kipindi kizima cha kwanza, lakini dakika ya 64, Edin Dzeko alifunga bao la
kuongoza na dakika nane baadaye aliongeza bao la pili.
Stevan
Jovetic aliyetokea benchi aliihakikishia ushindi Man City baada ya kufunga bao
la tatu dakika ya 86, kabla ya Yaya Toure kuhitimisha karamu ya mabao dakika za
nyongeza.
Pellegrini
ameipongeza timu yake kwa kucheza vizuri na kupata ushindi na sasa kuhitaji
pointi moja tu kuchukua ubingwa kwasababu ya wastani mzuri wa magoli.
“Timu
haikuvumilia tu, tulicheza vizuri”. Pellegrini ameiambia BBC Sport.
“Tulimiliki
vizuri mpira. Tulijitahidi kukaa na mpira na kwenda mbele kwa kasi kadri
tuwezavyo na tulitengeneza nafasi mbili au tatu kipindi cha kwanza”.
“Nilikuwa
na uhakika kuwa kama tutaendelea kucheza vile tungepata nafasi za kufunga
magoli”.
“Sasa
tunaweza kuzungumzia ubingwa. Lazima tushinde mechi ya mwisho dhidi ya West Ham”.
0 comments:
Post a Comment