MSHAMBULIAJI
wa Manchester City, Sergio Kun Aguero kwa asilimia 100 anaamini atacheza mechi ya
mwisho ya ligi kuu soka nchini England jumapili dhidi ya West Ham, hata kama
atakuwa na maumivu.
Nyota
huyo raia wa Argentina alipata majeruhi kwenye mechi dhidi ya Everton na kukosa
mechi ya katikati ya wiki dhidi ya Aston
Villa ambayo City walishinda mabao 4-0.
Wastani
mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa yanawafanya City wahitaji sare ili kutwaa
ubingwa, huku Aguero akisema lazima achangie ushindi Etihad jumapili.
“Najisikia
vizuri- lakini kwa asilimia 100 siko fiti, jumapili lazima nicheze,” nyota huyo mwenye
miaka 25 ameiambia tovuti ya klabu.
“Hata
kama sitakuwa fiti, umuhimu wa mechi hii ambayo kila mtu anatamani kucheza
utanifanya niingiae uwanjani na sitasikia maumivu”.
Aguero
sio mgeni katika kuamua matokoe kwa mechi za mwisho na msimu wa 2011/2012
alifunga bao lililowapa ubingwa Man City dhidi ya QPR, lakini nyota huyo
amesema West Ham hawatakuwa sawa na QPR waliokuwa wanapambana kukwepa kushuka
daraja.
“Nadhani
itakuwa tofauti, lakini haimaanishi itakuwa kazi rahisi”. Aliendelea.
“Wana
nguvu nzuri-West Ham wanakuja Etihad kwa malengo ya kutufunga, lakini hawana
presha yoyote, kwahiyo mechi itakuwa tofauti”.
“Sisi
tuko katika presha ileile kama wakati ule kwasababu tunahitaji kushinda ili
kutwaa ubingwa”
0 comments:
Post a Comment