Kocha wa Nigeria, Stephen Kheshi |
SHIRIKISHO la Soka Nigeria (NFF) limetangaza kikosi cha cha awali cha
wachezaji 30 kwa ajili ya Fainali za Kombe la Dunia la FIFA nchini Brazil
baadaye mwaka huu.
Kutangazwa kwa wachezaji hao jana, kumefutia kikao cha pamoja baina ya NFF
na kocha wa Super Eagles, Stephen Keshi.
Kikosi hicho ni makipa; Vincent Enyeama, Austin Ejide, Chigozie Agbim na
Daniel Akpeyi; Mabeki: Elderson Echiejile, Juwon Oshaniwa, Godfrey Oboabona,
Azubuike Egwuekwe, Kenneth Omeruo, Joseph Yobo, Kunle Odunlami na Efe Ambrose.
Viungo: John Mikel Obi, Ogenyi Onazi, Ramon Azeez, Joel Obi, Nosa Igiebor,
Michael Uchebo, Ejike Uzoenyi, Sunday Mba na Reuben Gabriel, wakati
washambuliaji ni: Ahmed Musa, Shola Ameobi, Emmanuel Emenike, Obinna Nsofor,
Osaze Odemwingie, Babatunde Michael, Victor Moses, Uche Nwofor na Nnamdi
Oduamadi.
Nigeria ni moja kati ya nchi tano za Afrika zitakazoshiriki fainali za Kombe la dunia mwaka huu, pamoja na Algeria, Ghana na Ivory Coast.
Nigeria ni moja kati ya nchi tano za Afrika zitakazoshiriki fainali za Kombe la dunia mwaka huu, pamoja na Algeria, Ghana na Ivory Coast.
0 comments:
Post a Comment